ABDULRAHMAN KINANA WA CCM, NI MWIBA MKALI AIBOMOA NGOME YA CHADEMA IRINGA,AMCHUKUA KIGOGO MZITO WA CHADEMA, SOMA HAPA KUMJUA

Soda akikabidhi kadi yake ya Chadema kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya uamuzi wake wa kuamua kuhamia CCM kwenye mkutano huo.

Kinana akionyesha kadi ya Soda na vijana wengine 27 waliohamia CCM kumfuata Soda.(Martha Magessa)

Soda akizungumza mbele ya Kinana. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenzi nape Nnauye aliyefanyakazi ya kumkaribisha Soda jukwaani.

Vijana walioamua kumfuata Soda kuhamia CCM wakionysha kadi zao za Chadema kabla ya kumkabidhi Kinana

Kinana akimkabidhi Soda kadi ya CCM. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iriga, Jesca Msambatavangu

Kadi mpta ya CCM aliyokadhiwa Soda

Vijana waliomfuata Soda kuhamia CCM wakipewa kadi za CCM na Kinana

Wananchi wakishangilia baada ya Kinana kumpokea Soda na vijana hao

Soda (kulia) akiungana na wenzake kula kiapo baada ya kukabidhiwa kadi za CCM na Kinana

Baadhi ya waandishi wa habari walioko kwenye msafara wa Kinana mkoani Iringa, wakiwa kwenye mnara uliojengwa na Soda kwa ajili ya kumbukumbu ya Mwangosi. Hata hivyo mnara huo hauna maandishi wala chochote kinachoonyesha kuwa umanhusu marehemu Mwangosi

Kiongozi wa bendi ya CCM ya Mafinga, akiongoza kuimba wimbo maalum wa CCM inavyotekelza ilani ya Uchaguzi, wakati wa mkutano huo

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana (kulia) akiungana na wananchi kuselebuka wimbo huo maakum wa CCM

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwa na wanamuziki wa bendi hiyo ya CCM baada ya wimbo huo

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana na Nape wakiitazama albamu ya wimbo huo maalum wa CCM. Picha zote na Bashir Nkoromo-theNkoromo Blog

Katibu wa Chadema Kata ya Igowole, wilayani Mufindi mkoani Iringa, Josephat Soda akitangaza kukihama chama hicho, mbele ya maelfu ya wananchi katika mkutano wa hadhara wa Kinana uliofanyika leo, Oktoba 10, 2014, kwenye mjini mdogo wa Nyololo. Soda amesema ameamua kukihama chama hicho baada ya kubaini kuwa ni matapeli waliompa kazi ya kujenga mnara wa kumbukumbu wa mwandishi wa habari David Mwangosi, aliyeuawa katika mapambano cha Chadema na Polisi wakati wa maandamano yaliyofanywa na chama hicho mwaka juzi katika mji huo mdogo wa Nyololo ambapo aliujenga mnara huo wa gharama zake na kukopa saruji kwa ahadi ya kulipwa na viongozi wa Chadema lakini hadi leo ameambilia patupu.
No comments
Post a Comment