MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE---SERIKALI YA TANZANIA INATAFUTA KINGA YA KUWAKINGA WANAOFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE.SOMA HAPA UJUE KWANINI
Na Karoli
Vinsent
SERIKALI Imesema
iko mbioni kutafuta njia itakayoweza kuwasaidia watu wanaofanya mapenzi ya kinyume
na maumbile ili waweze kujikinga na magonjwa mbalimbali.
Kauli hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam, na Mganga
mkuu wa Serikali Dkt.Donnan Mbando wakati wa mkutano na waandishi wa Habari
katika mkutano huo uliandaliwa mahususi kwa ajili ya kuzungumzia kuhusu mkutano
wa 20 wa Kimataifa wa Ukumwi Duniani uliofanyika mwezi wa saba mwaka huu nchini
Melbourne nchini Austaria.
Ambapo alisema kwa sasa serikali ya
Tanzania iko mbioni kutafuta njia ya kuwasaidia watu wanaofanya mapenzi kinyume
na maumbile ili wasiweze kupata magonjwa.
“Na sasa serikali inatafuta njia ya kuweza kuwakinga
watu wanaofanya Mapenzi kinyume na maumbile ili waweze kujikinga na magonjwa
kwani tumegundua katika mkutano huo kwamba sababu inayopelekea maambukizo ya
ukimwi yanatokana na watu kufanya mapenzi kinyume na maumbile sasa imekuwa ni kubwa,na sasa tumegundua watu hao
hawezi kuacha “alisema Mbando.
Kwa upande wake Mwenyekiti
Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti
UKIMWI Tanzania TACAIDS Dkt Fatma Mrisho alisema wao wamejipanga kuwapa elimu
Madaktari na wahudumu wengine wa afya iliwaweze kuwapa huduma za Afya bila ya
kuwatenga watu wanaofanya mapenzi kinyume na Maumbile.
“Mwaka jana katika Ripoti ya Haki za
Binadamu ilikuwa inasema Tanzania inawanyapaa watu wanaofanya mapenzi ya Jinsia
moja,nataka niwambie sio
kweli Tanzania haiwatengi watu wanaofanya mapenzi ya jinsia Moja ambapo sio
kweli kabisa,na sasa tume yangu iko mbioni kuwapa elimu wa wahudumu wa Afya
wasiwanyapae watu hawa”alisema Dkt Mrisho.
No comments
Post a Comment