KUMEKUCHA BUNGE LA KATIBA---WAZIRI LUKUVI AWAVAA UKAWA,ASEMA BUNGE LA KATIBA LITAENDELEA KAMA KAWA NA KATIBA ITAPATIKANA BILA HATA YA UKAWA SOMA HAPA UJUE KWANINI
Pichani ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu na Bunge, Willium Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo bunge la katiba
Na Karoli
Vinsent
HUKU ikiwa
bado wingu limetawala kuhusu hatma ya upatikanaji wa katiba Mpya,kutokana na upande umoja unaojiita
Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) kususia vikao vya Bunge Maalum la katiba na
kusema hawatarudi kwa kile wananchokiita Mchakato huo unafanyiwa Hujuma na
Chama cha Mapinduzi CCM.
Naye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu na Bunge, Willium Lukuvi amezidi kulichanganya Taifa baada ya
kusema Vikao vya Bunge maalum Vitaendelea hata kama Upande mwengine wa UKAWA
wasiporejea kwenye Bunge hilo.
Kauli hiyo ameitoa leo Ikulu Jijini Dar Es Salaam wakati wa Mkutano
na Waandishi wa Habari,ambapo kauli hiyo ya Waziri Lukuvi inakuja huku kukiwa
imebaki siku moja kabla ya Vikao vya Bunge Maalum la katiba Vitakavyoanza Kesho
Mkoani Dodoma.
Waziri Lukuvi alisema kwa sasa
wanakwenda Dodoma kujadili sura
zilizobakia ambazo amesema zinawahusu watanzania zaidi kuliko sura zilizopita.
“Kwanza niseme kwamba Vikao vya Bunge
maalum vitaendeleo kama kawaida na hapa mnaponiona mimi nikimaliza kuongea na
nyinyi nakwenda moja kwa moja Mkoani Dodoma,na ikumbukwe tunakwenda kumalizia
sura zilizobakia maana katika kipindi kile cha kwanza tulijadili sura mbili tu
na sahivi tunakwenda kujadili sura zaidi ya tisa zilizobakia na tunakwenda bila
uwoga na kwamba kwanini UKAWA hawapo sisi hiyo sio tatizo”Alisema Lukuvi.
Waziri Lukuvi,ambaye ni Mbunge wa jimbo la Isimani CCM
alizidi kusema wao hawashitushwi na kutokuwepo kwa UKAWA,kwani wajumbe
waliobakia wanaweza kutunga katiba na haina haja ya kuwasubili watu wasiokuwa
na tija juu ya upatikani wa katiba Mpya.
Katika hatua nyingine nao
Wajumbe mbalimbali waliokuwepo kwenye iliyokuwa Tume ya katiba ya ukusanyaji wa
maoni ya wananchi,waliokuwa wakinzungumza kwenye mdahalo uliofanyika leo Jijini
Dar es Salaam ambao mdahalo huo ulirushwa moja kwa moja kwenye kitua cha ITV.
Ambapo walisema mchakato
huo wa Katiba umehalibiwa na Rais Jakaya
Kikwete kutokana na kuwadanganya wananchi kuhusu upatikani wa katiba mpya.
Kwa upande wake Mjumbe aliyekuwapo kwenye
iliyokuwa tume ya Ukusanyaji wa Maoni Hawadh Ally alisema ameshindwa kuelewa
elimu ya masuala ya uchumi aliyekuwano Rais Jakaya Kikwete kwa kitendo chake
cha kusema muundo wa Serikali tatu ni mzigo.
No comments
Post a Comment