JUKWAA LA KATIBA :RAIS WANGU KIKWETE USIJIFICHE NYUMA YA HAO CCM, JITOKEZE UOKOE MABILIONI HAYA YA WALALAHOI
| Kaimu mwenyekiti wa jukwaa la katibaBw. Hebron Mwakagenda Akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari huko ofisini kwake |
Jukwaa
la katiba Tanzania JUKATA limefanikiwa kupenya na kuingia katika bunge
la katiba na kukutana na kamati zote kumi na mbili, ambapo katika kamati
hizo wamebaini mapungufu makubwa ambayo yanatia shaka upatikanaji wa
katiba mpya inayoendelea kujadiliwa huko mjini Dododma,
Akizungumza
na mwandishi wa mtandao huu mapema hii leo,Kaimu mwenyekiti wa jukwaa
la katiba Tanzania Bw. Hebron Mwakagenda, amsema katika safari yao hiyo
wamebaini mambo makubwa kumi ambayo yanatia shaka kwa katiba mpya ya
jamuhuri ya muungano wa Tanzania kupatikana,
Mwakagenda
amesema kwanza kabisa achilia mbali idadi ya wabunge ambao hawajitia
mguu katika bunge hilo toka kuanza kwa awamu ya pili ,lakini lokoo
inaonyesha kuwa wabunge wengi hawahudhilii vikao vya kujadili rasmu ya
katiba,
Amesema
tokea kuanza kwa vikao hivyo, Wabunge wengi wamekuwa hawahudhulii
vikao, kwa sababu hawahudhulii vikao basi kamati inaamua kufanya kikao
hicho kama semina ili waende kula kodi za watanzania bure huku wakijua
wazi kufanya hivyo ni ubadhilifu wa mali ya umma,
Wamekuwa
wakibali vikao kuwa semina hiyo ni kutokana na akidi kutotimia, sasa
wanaamua kujitengenezea mazingira ili waendelee kupiga psa za walala hoi
| Mwakagenda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mapema hii leo. |
Katika
hatua nyingine Mwakagenda ameibua ufisadi mwingin unaofanywa na
mawaziri katika bunge hilo la katiba kwa kusema , mawazili hao wamekuwa
wakijitengenezea mazingira ya kutohudhuria vikao lakini bado posho zao
zikiendelea kumiminika katika akaunti zao
Mawaziri
wanatakiwa kutoa taarifa kwa waziri mkuu juu ya udhulu wao, lakini
wanapofanya hivyo bado fedha zao zinaendelea kuingia katika akaunti zao
wakati wao wanafanya kazi tofauti na kutunga katiba, amesema ilie ni
sehemu yao ya kazi kwa nini sasa bunge la katiba liwalipe pesa huku
wakifanya kazi nyingine Alihoji
SABU TATU MUHIMU KIKWETE KUNUSURU MCHAKATO WA KATIBA
- Mahudhulio hafifu ya wajumbe wa bunge la katiba, hakuna wajumbee kiasi kwamba wachumia tumbo wachache wameamua kubadili vikao hivyo kuwa semina za kujipatia kipato,. LOkoo zinadaiwa kutotimia kwa kila kamati na hivyo wanaamua kubadili vikao kuwa semina za kujaziana uwezo, alipohojiwa na jukata, mwenyekiti wa bunge hilo alikili hadharani kuwa akidi hazitimiii
- Kukosekana kwa muafaka wa malidhiano, hii ni sababu muhimu sana kwani mpaka sasa kuna sauti nyingi toka kila kona ya nchii hii ikisema bunge hilo lisimame kwanza kwani kuna miradi mingi ya kufanya kwanza, mpaka sasa watu wengi hawaridhika na kuendelea kwa vikao vya tume hivyo, hivyo rasi anaombwa kuingilia mchakato kunusuru mabilioni ya walipa kodi,. Alipoulizwa na mwandishi wa mtandao huu kuhusu uweezo wa rais kuingilia kati mchakato, Mwakagenda alisema ni kweli rais hana mamlaka ya kuvunja bunge hilo lakini pia ni kweli kuwa rais hana malakaya kuanzisha mchakato wa kutunga katiba mpya, kwa sababu amelianzisha ni lazima basi busara zitumike pia kulimaliza,. Tunajua kuwa rais alikuwa na nia nzuri ya kutupatia katiba lakini kutokana na sababu ambazo hazizuiliki basi rais wtu kipenzi aangalienamna ya kutusaidia kuokoa mabilioni haya ya shilingi yanayotumika huku tukijua wazi kuwa katiba mpya haipatikaniki
JUKATA LATOA MSIMAMO WAKE
Jukata linataka mchakato wa katiba mpya usimame upishe michakato mingine ya kitaifa tena yenye uzito mkubwa kama wa uandikishaji wa vitambulisho vya kitaifa, uandikishaji wa wapika kura, kwenye daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa kielectroniki (BVR),Uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwakati ambao miradi yote hiyo inahitaji pesa nyingi za kufanikisha kwake
No comments
Post a Comment