Zinazobamba

wasomi vyuo vikuu wafafanua kushindwa kwa Chadema, wasema Mbowe hashauriki

GRACE MERERE, MMOJA WA WAPIGANAJI AKIPOZI MBELE YA MWANDISHI WA HABARI HIZI, MERERE AMESEMA LAZIMA SUBRA INAHITAJIKA ILI CHAMA KUJENGA MIZIZI YAKE

Ushindi wa chama cha mapinduzi katika jimbo la Kalenga uliofanyika hivi karibuni umeelezewa kuwa ni ishara kuwa kuna kazi kubwa ya kufanya ili kukiondoa chama Tawala kwa miaaka mingine 20 ijayo,

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni katika mahojiano maalum, wanafunzi wa vyuo vikuu hapa nchini wamesema kuwa, kushindwa kwa chadema katika uchaguzi huo wa Kalenga haina maana kuwa Chadema haikubaliki katika Jimbo hilo, bali kuna kazi kubwa ya kufanya ili mbegu kwa maana watoto wadogo, waweze kuamini kuwa Chadema ndio mkombozi wao wa maisha yao,



Akifafanua zaidi Mmoja wa wanafunzi hao alijitambulisha kwa jina la Grace Merere, anasoma katika chuo cha taifa cha usafirishaji fani ya logistics na usafirishaji, amesema watu lazima wafahamu kuwa chadema inajengwa mizizi,ukizingatia kuwa CCM mpaka sasa kina miaka mingi tokea 1973, hali inaoonyesha kuwa kuna miaka mingine 20 ili vizazi vyetu viweze kubadilisha mfumo wa maisha kwa kukiondoa Chama cha Mapinduzi,

Akizungumzia, namna ya uongozi wa kurithishana unaendelea katika taifa hili la Tanzania, Merere amesema hakuna utaratibu mbaya ambao unakera kama kuona watoto wa watawala wanarithishwa madaraka kama kwamba taifa hili limekosa watu wa kuwatumikia wananchi, 

Amesema hivi kweli Tanzania tumekosa watu wa kuwaweka mpaka tuweke watoto wa kinabwana mkubwa, Ukweli inakera sana lakini ndiyo hivyo inatubini kizazi hiki caha ccm kipite ndipo tufanye mageuzi kupitia vizazi vipya vijavyo

Katika hatua nyingine, baadhi ya wadau mbalimbali waliohojiwa na Mtandao huu kufuatia kushindwa kwa chadema katika chaguzi iliyofanyika huko kalenga, wadau mbalimbali wamebainisha sababau zilizofanya chama hicho kushindwa kwa kishindo,
Miongoni mwa Sababu zilizotajwa kwa chama hicho kushindwa ni Pamoja na Mwenyekiti wa Chama hicho kushindwa kushaurika baada ya kubaini wazi kuwa daftari la wapiga kura lilikuwa halijafanyiwa marekebisho, hivyo wasingeweza kushinda kwani vijana wengi walikuwa hawana shahada za kupigia kura,
Sababu zingine ni kwa kwamba chama kimetumia pesa nyingi kurusha chopa, wakati pesa hizo zingetumika katika kujenga chama kwa kutambua changamoto zinazowakabili wana kalenga na kuwatatulia ili kujenga jina kwa wanakalenga,

Chadema wangeweza kujenga Visima vya maji sfi ili wanakalenga wajue kuwa kuna mkombozi anaumia kwa sababu ya ustawi wa maisha yao, lakini inashangaza kuona hela nyingi zimetumika katika eneo ambalo halina tija Kwa Chama wala wanakalenga wenyewe

1 comment

Anonymous said...

Ugumu wa kushauriwa siyo wa Mbowe tu, hata Slaa na toto Tundu