Zinazobamba

uchaguzi jimbo la kalenga ni jino kwa jino, hawahapa ccm nao, wapiga kampeni kijiji kwa kijiji....habari kamili hii hapa

Kalenga,Wananchi Waendelea kufurika kwenye Mikutano ya CCM,Mwigulu afanya kampeni za Kijiji Kwa Kijiji

Naibu Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wanakijiji wa Kibebe hii leo wakati wa kumnadi Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Godfrey William Mgimwa.Hii leo Mwigulu Nchemba ameendesha mikutano minne kwenye Vijiji Vinne tofauti(Mwambao,Kibebe,Lupalama na Mangali).Katika Vijiji Vyote Wananchi wamejitokeza kwa wingi sana na hakika Wameahidi kuiunga mkono CCM hasa kutokana na maendeleo waliyoyapata tangu awali kwa Mbunge aliyefariki.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na
Wanakijiji wa Kijiji Cha Mwambao hii leoKijiji cha Mwambao Vijana wakishangilia na Kumpokea Mgombea wa Ubunge Jimbo la Kalenga wa CCM,Godfrey William Mgimwa.Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Mangali hii leo kata ya kalenga
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na wanakijiji wa Kibebe Jimboni kalenga hii leo.
 Kada Mtiifu Mtela Mwampamba akizungumza na Wananchi wa Kata ya Kibebe wakati wa kumnadi Mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Godfrey William Mgimwa hii leo.
Mapokezi mazito Kata ya Kibebe kwa Godfrey Mgimwa mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga.

No comments