TUZO ZA MCT NI UBABAISHAJI MTUPU,YAWAGAWA WAANDISHI VIPANDE VIPANDE, WAANDISHI WENGINE WASEMA KUNA HAJA YA KUWA NA BALAZA LA HABARI LA TAIFA NA SIO HII NGO
![]() |
|
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la
Habari (MCT), Pili Mtambalike akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari, Mtambalike alisema mchujo huo umefanywa na jopo la
majaji lililoongozwa na mkufunzi na mhariri wa habari wa siku nyingi
nchini, Gervas Moshiro.PICHA|MAKTABA
|
SIKU MOJA BAADA YA BALAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) KUTANGAZA MAJINA YA WAANDISHI WALIOINGIA KATIKA HATUA YA MWISHO YA KUWATANGAZA WASHINDI WA UANDISHI MAKINI KATIKA KATEGOLI MBALIMBALI HAPA NCHINI, KUNDI KUBWA LA WAANDISHI HAPA JIJINI WAIMEBUKA NA KULITUPIA LAWAMA BALAZA HILO KUWA KATIKA KUCHUJA KAZI ZAO KULIKUWA NA UPENDELEO MKUBWA
UTAFITI ULIFANYWA NA MWANDISHI WA HABARI HIZI UKIWASHIRIKISHA WAANDISHI MAKINI NA WA SIKU NYINGI, UMEBAINI KUWA LAWAMA NYINGI ZINAELEKEZWA KATIKA BALAZA HILO KWA KUWA HAWAKO TAYARI KUWATAJA WAANDISHI WANAOSHINDA NA KAZI YAKE ILIYOMFANYA ASHINDE ILI WADAU WA SEKTA HIYO KUJIRIDHISHWA NA KAZI HUSKA,
WAKIZUNGUMZA KATIKA MAHOJIANO MAALUM KATIKA HOTEL YA BLUEPEARL MAPEMA HII LEO, WAANDISHI AMBAO HAWAJAPENDA KUTAJWA KATIKA MAKALA HAYA, KUTOKA KATIKA MAGAZETI MBALIMBALI NA REDIO, WAMESMA KAMA MCT WATAAENDELEA NA UBABAISHAJI WAO WANAUENDEKEZA ITAFIKA WAKATI KILA MWANDISHI ATASUSIA KUPELEKA KAZI ZAKE KATIKA BALAZA HILO KUFUATIA KUTOKUWA NA IMANI NALO,
WAANDISHI HAO WAMEENDA MBELE ZAIDI NA KUSEMA KINACHOONEKANA KWA SASA PALE MCT NI KWAMBA WATU WAPO KWA MASLAHI YAO NA TAYARI WAMESHAMPANGA MTU WAO ILI AWEZE KUSHINDA TUZO HAPO MARCH 14.
UKIANGALIA KWA MAKINI UTEUZI WAO UMEKUWA BIAS SANA, HATUJI HATA HABIBU ZA REJEA WANAZOTUMIA KUMPA MTU USHINDI, .... BASI HATAKAMA MTU AMEFANYA VIZURI NA KUPELEKEA KAZI YAKE KUSHINDA BASI HIYO KAZI ITAJWE ILI WADAU TUPIME HIYO KAZI KAMA NI KWELI INASTAHILI KUSHINDA AMA VIPI TUPIGE KURA YA KUTOKUWA NA IMANI NAYO
MWANDIHSI MMOJA TOKA KAZETI LA KILA LEO, AMEBAINISHA WAZI KUWA YEYE MWENYEWE AMEPELEKA MAKALA YASIYOPUNGUA 7 AMBAYO KWA KATEGOLI YAKE ISINGEKUWA VIGUMU KWA KAZI HIZO HATA MOJA ISHINDWE KUPITA, KITU AMBACHO ANADAI KUNA MTU TAYARI AMEPANGWA KUSHINDA TUZO ZA MWANDISHI BORA MWAKA HUU,
SASA NADHANI SERIKALI KUNAHAJA YA KUANZISHWA CHOMBO MAKINI KITAKACHOSHUGHULIKIA MIGOGORO KAMA HII, WE HUWEZI KUWAACHIA MCT PEKE YAO AMBAO SIYO TAASISI YA SERIKALI HIVYO INAWEZA KUAMUA KUTOKANA NA MATAKWA YA MABOSI WAO, ALIONGEZA MWANDISHI MWINGINE TOKA TSN.
Dar es Salaam. Waandishi wa Habari wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi, Mwanaspoti na The Citizen wanaongoza katika orodha ya wateule wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari 2013 (Ejat 2013) kwa kuingiza majina 15 kati ya 76 ya wateule watakaotunukiwa zawadi zao Machi 14 mwaka huu.
Akizungumza wakati wa hafla ya kutaja majina ya wateule hao, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Taifa la Habari (MCT), Pili Mtambalike alisema mchujo huo umefanywa na jopo la majaji lililoongozwa na mkufunzi na mhariri wa habari wa siku nyingi nchini, Gervas Moshiro.
Mtambalike alisema washindi watatunukiwa tuzo zao na Rais wa Mahakama ya Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jaji Harold Nsekela katika hafla itakayofanyika Machi 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Jumla ya kazi 907 ziliwasilishwa kwa ajili ya kuwania tuzo hizo.
Alisema majaji walizipitia na kupitisha kazi 101 ambazo ni pamoja na za magazeti (46), redio (39) na televisheni (16) na kulingana na takwimu hizo, idadi ya kazi za redio imeongezeka kutoka 21 za mwaka 2012 na magazeti kazi tano zaidi zimeongezeka
Kazi za televisheni zimepungua kwa idadi ya tatu kutoka 19 za mwaka 2012. Idadi ya kazi zilizopitishwa katika mchujo wa majaji hao zimeongezeka kutoka 76 hadi 81, kiwango ambacho ni sawa na ongezeko la asilimia 24.6.
Mtambalike alisema pia idadi ya washiriki wanawake nayo imeongezeka kutoka washiriki 12 hadi 18 kwa mwaka 2013, ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 63.6. Alisema ili majaji kuwapata wateule hao walilazimika kufanya kazi ya ziada kutokana na ushindani uliokuwepo.
Kwa upande mwingine, kaimu mkurugenzi huyo alisema, jopo la wataalamu chini ya uenyekiti wa mhariri wa siku nyingi na mtalaamu wa masuala ya habari, Theophil Makunga, bado lipo katika mchakato wa uteuzi wa jina linalostahili kushinda Tuzo ya Maisha ya Mafanikio na Uandishi wa Habari (LAJA).
Waandishi wa Magazeti ya Mwananchi na The Citizen ambao majina yao yametajwa katika wateule wa tuzo hizo kwa mwaka 2013 ni pamoja na Fred Azzah, Florence Majani, Polycarp Machira, Kalunde Jamal, Herieth Makweta, Beldina Nyakeke, Sheilah Sezzy, Elias Msuya, Jacqueline Masinde na Athuman Mtulya.
Wengine ni Fidelis Felix, Kelvin Matandiko, Phinias Bashaya, Zephania Ubwani, Mussa Juma.Waandishi hao wa MCL wameongezeka kwa idadi ya mwandishi mmoja ikilinganishwa na idadi ya wateule 14 wa tuzo zilizopita.

No comments
Post a Comment