Zinazobamba

Tigo sasa baba lao, yaweka historia nyingine ya kutuma pesa nje ya mipaka ya nchi, yanza na Kigali

  
Kampuni ya mawasiliano ya TIGO TANZANIA leo imeweka historia nyingine ya dunia baada ya kuzindua huduma yake mpya ambayo sasa unaweza kutuma na kupokea pesa  ukiwa nchini Rwanda na Tanzania kwa kutumia tigo pesa kwa Tanzania na tigo cash kwa Rwanda  Huduma hiyo ambayo imezinduliwa leo katika tafrija mbili tofauti moja ikiwa Tanzania na nyingine ikiwa Rwanda inatajwa kuwa ya kwanza kufanyika duniani kwani katika huduma hiyo  unaweza kupokea pesa za nchi husika kama zilivyotumwa

 
BALOZI WA RWANDA BEN RUGANGAZA AKIWASILIANA NA BALOZI WA TANZANIA NCHINI RWANDA WAKATI AKIMTUMIA HELA KWA TIGO PESA KWA MARA YA KWANA KATIKA HUDUMA HIYO AMBAYO IMEZINDULIWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM NA MUDA HUOHUO IKIZINDULIWA NCHINI RWANDA 

 Huduma hiyo ilishuhudiwa na balozi wa Rwanda nchini Tanzania bw BEN
RUGANGAZA pamoja na balozi wa Tanzania nchini Rwanda,ambapo wote kwa pamoja wameipongeza kampuni ya tigo kwa kufanikisha huduma hiyo ambayo inatajwa kuwa ya kwanza kutokea Tanzania na duniani kwa ujumla. 
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa tigo Tanzania DIEGO GUTIEREZ amesema
kuwa baada ya mteja kupokea pesa ikitokea baina ya nchi hizo mbili mteja anaweza kuitumia kulipia huduma zote za tigo zinazopatikana katika tigo pesa au tigo cash kwa Rwanda.   Amesema kuwa huduma hii itaokoa muda mwingi sana ambao wateja wake wanchi hizo mbli walikuwa wanaupoteza katika kutuma pesa huku akitaja jinsi ya kuipata huduma hiyo kuwa ni *150*90#  ka Tanzania huku wale walioko Rwanda wakipiga *200*7#.




No comments