PICHA INATISHA..UKATILI TABORA..AMCHINJA MKEWE KISA KUNYIMWA UNYUMBA NAYE AJIKATA KOO NA KUNUSURIKA..!
Mkazi wa mmoja wa Nzega, mkoani Tabora, Juma Kiyabo (45) amemchija mke wake, Wande Monera (34), kabla ya mwenyewe kunusurika kifo baada ya kujijeruhi vibaya shingoni katika jaribio la kutaka kujiua.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Tazengwa saa 7 usiku wa Februari 16
mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba mara
kwa mara.
Kaimu Kamanda wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu Msaidizi mkoani Tabora, John Kauga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kaunga alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa alikuwa akigombana na mkewe mara kwa mara kwa sababu ya kunyimwa unyumba kabla ya kuamua kuchukua hatua hiyo mbaya.

No comments
Post a Comment