• Home
  • About Us
  • Contact Us
  • Advertise

Full Habari
ads header
    • KITAIFA
    • KMATAIFA
    • BIASHARA
    • SIASA
    • MICHEZO
  • Zinazobamba

    Home / Unlabelled / Zitto Kabwe amvimbia mwanasheria mkuu wa Serikali....Adai kuwa mwanasheria ni muongo mkubwa.. Yeye alishampa majina muda mrefu sana

    Zitto Kabwe amvimbia mwanasheria mkuu wa Serikali....Adai kuwa mwanasheria ni muongo mkubwa.. Yeye alishampa majina muda mrefu sana

    Full habari Digital 18:14:00
    MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), amesema atamjibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema juu ya kauli aliyoisema bungeni kwamba mbunge huyo hana majina ya Watanzania walioficha mabilioni ya fedha nchini Uswisi. Zitto alisema kwa kuwa Jaji Werema alimshambulia kupitia bunge naye atatoa majibu bungeni ili ukweli uweze kujulikana.


    Zitto alitoa kauli hiyo jana nje ya ukumbi wa Bunge alipokuwa akizungumza na Rai iliyotaka kujua msimamo wake baada ya Jaji Werema kuliambia Bunge Zitto aliiambia kamati iliyoundwa na Serikali kuchunguza sakata la Watanzania wanaodaiwa kuficha fedha nje ya nchi kwamba hana majina.

    “Nilimsikia Mwanasheria MKuu wa Serikali akinishambulia jana (juzi), nitakachokifanya ni kwamba wiki ijayo nitamjibu hapa bungeni baada ya kumuomba Spika anipe nafasi ya kuwasilisha maelezo binafsi.

    “Mwanasheria Mkuu ni muongo, nasema totally ni muongo kwa sababu kwenye kamati yao nimehudhuria mara nne na nikawakabidhi majina ya watuhumiwa.
     

     “Tena kibaya zaidi, niliwakabidhi mpaka jina la mchunguzi wa kimataifa anayeweza kuwasaidia katika uchunguzi wao, halafu leo anasema nilikuwa naikwepa kamati ni muongo, nasema ni muongo, lakini, hoja iliyopo ni je, mabilioni yapo au hayapo,” alisema Zitto kwa kifupi.

    Juzi, Jaji Werema aliliambia Bunge jinsi ambavyo Zitto alikuwa akikwepa kutoa taarifa za watu walioficha fedha nchini Uswisi.

    Jaji Werema alisema licha ya mbunge huyo kukaririwa mara kadhaa akisema anayo majina ya walioficha fedha hizo nje ya nchi lakini mara kadhaa alikuwa akikwepa kuhojiwa na kamati iliyoundwa na Serikali kufuatilia fedha hizo.

    Alisema kutokana na tabia hiyo Serikali imeazimia kuchukua hatua za kisheria dhidi yake na kusisitiza hawawezi kukubali mtu alidanganye Bunge.

    Jaji Werema alisema hayo alipokuwa akihitimisha mjadala wa taarifa ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala.

    “Lakini leo hapa amesema Serikali haina nia ya kurudisha fedha
    zilizofichwa Uswisi, kwa maana hiyo Mheshimiwa Naibu Spika, Zitto Kabwe ni mzito na nakubaliana na Lema (Mbunge wa Arusha Mjini) aliyesema hapa kwamba Zitto alete majina hayo,” alisema Jaji Werema.
    -MTANZANIA
    Zitto Kabwe amvimbia mwanasheria mkuu wa Serikali....Adai kuwa mwanasheria ni muongo mkubwa.. Yeye alishampa majina muda mrefu sana       Zitto Kabwe amvimbia mwanasheria mkuu wa Serikali....Adai kuwa     mwanasheria ni muongo mkubwa.. Yeye alishampa majina muda mrefu sana Reviewed by Full habari Digital on 18:14:00 Rating: 5
    Share This
    Facebook Twitter Google+

    No comments

    Post a Comment

    Subscribe to: Post Comments ( Atom )

    Ads

    Popular Posts

    • MATOKEO YA MTIHANI HAYA HAPA NI YALE YALIOTANGAZWA NA NECTA LEO,BOFYA HAPA KUJUA
    • MIZENGO PINDA AMUHURUMIA MBUNGE KAWAWA,HALI YAKE YASHTUA WENGI TIZAMA PICHA HIZI
      MIZENGO PINDA AMUHURUMIA MBUNGE KAWAWA,HALI YAKE YASHTUA WENGI TIZAMA PICHA HIZI
    • WAISLAM WAONYWA,WAAMBIWA MANENO KUNTU,SOMA HAPA KUJUA
      WAISLAM WAONYWA,WAAMBIWA MANENO KUNTU,SOMA HAPA KUJUA
    • DIWANI KATA YA BUYUNI AZUNGUMZIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NDANI YA SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA.
      DIWANI KATA YA BUYUNI AZUNGUMZIA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO NDANI YA SIKU 100 ZA RAIS DKT. SAMIA.

    Total Pageviews

    Recent Posts

    Tangazo

    Labels

    • Afya
    • Biashara
    • Burudani
    • Dini
    • Elimu
    • Jamii
    • Kijamii
    • Kimataifa
    • Kitaifa
    • Mahakama
    • Michezo
    • Siasa

    Facebook

    Followed Blogs

    • Michuzi
    • Dar24
    • MPEKUZIHURU

    KWA MATANGAZO

    WASILIANA NA UONGOZI WA FULLHABARI KUPITIA NAMBA ZIFUATAZO:

    0714 099 486
    0689 311 158

    Theme By Sora Templates | Designed By Mbinda Technologies (T) Ltd | Copyright © Beta Media Consultance Lmited