Zinazobamba

TANROADS KUSAINIWA KWA MIRADI MIKUBWA MITATU YA UJENZI WA BARABARA



11-Mk_wa_Mfuko_wa_Bodi_ya_Barabara_Dkt_James_Nyachia_kush_akimskiliza_mhandis_Ndukimana_kutoka_Tanrods_kulia_huko_Segerea_8bd30.jpg
Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mnamo siku ya Jumatatu ya tarehe 02 Desemba 2013 utasaini mikataba mitatu ya barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami katika mikoa ya Dodoma, Manyara na Mtwara.
Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli atakuwa Mgeni Rasmi katika hafla hiyo ya kusainiwa kwa mikataba ya ujenzi wa miradi hiyo mitatu mikubwa ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisubiriwa kwa hamu.
Miradi itakayohusika ni:
i. Mayamaya – Mela (km 99.35)
ii. Mela- Bonga (km 88.8)
Ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kuanzia Mayamaya hadi Bonga yenye urefu wa kilometa km 188.15 umegawanywa katika sehemu mbili ambazo zitakuwa na mikataba miwili tofauti inayojitegemea. Mikataba hiyo itajumuisha ujenzi wa sehemu ya Mayamaya – Mela (km 99.35) na Mela – Bonga (km 88.8).(P.T)
Kujengwa kwa sehemu hii kati ya Mayamaya na Bonga katika mikoa ya Dodoma na Manyara kutakamilisha barabara ya lami inayounganisha miji ya Dodoma na Babati kwa upande wa mkoa wa Manyara. Sehemu kati ya Dodoma – Mayamaya (km 43.6) ujenzi wake unaendelea kwa kiwango cha lami na kuanzia Babati hadi Bonga (km 19.2) tayari imekwishakamilika.
iii. Mangaka – Mtambaswala(km 65.5)
Kipande cha barabara kati ya Mangaka hadi Mtambaswala (km 65.5) mkoani Mtwara ni sehemu ya barabara inayoanzia Masasi hadi Mtambaswala (km 120.6) ambako kuna Daraja la Umoja linaounganisha nchi yetu na Msumbiji. Tayari sehemu ya kati ya Masasi na Mangaka (km 55.1) imekwishajengwa kwa kiwango cha lami na hivyo kusainiwa kwa sehemu hii ya Mangaka hadi Mtambaswala kutaifanya barabara hiyo yote kukamilika kwa kiwango cha lami.
Hafla ya kusaini mikataba hiyo mitatu itafanyikia Protea Court Yard Hotel, Ocean road, Upanga jijini Dar es Salaam kuanzia saa 4:00 asubuhi.

No comments