Polisi wakiondoka na mwili wa marehemu
MTU
mmoja asiyefahamika jina wala makazi yake, amepoteza maisha baada ya
kupigwa na
kuchomwa moto na wananchi ambao wameamua kujichukulia sheria mkononi.
Wananchi
hao ambao ni wakazi wa eneo la Mtakuja Mbalizi, walifanya tukio hilo
jana
majira ya saa mbili asubuhi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtakuja
Mbalizi Mbeya vijijini, Ambonisye
Masinga, alisema kuwa marehemu huyo alidaiwa kuiba pikipiki eneo la
Utengule.
Alisema,
baadhi ya madereva wa bodaboda(pikipiki) walianzisha msako na kufanikiwa
kumtia
nguvuni marehemu huyo na kuanza kumshushia kipigo huku mwili wake ukiwa
umefungwa kwenye pikipiki na kuuburuza barabarani umbali wa kilomita
moja.
Alisema,
mwili huo uliburuzwa na kufikishwa kwenye eneo la mlima reli maarufu kwa
jina
la eneo la adhabu kwa wahalifu na kuchoma moto mwili wake.
Aidha,
katika tukio hilo fundi ujenzi aliyekuwa katika eneo hilo Asangalwisye
Mayasu(50) mkazi wa kivukoni, alijikuta akiambulia kipigo baada ya
kujaribu
kuwazuia wananchi ambao waliamua kujichukulia sheria mkononi.
“Baada
ya msamalia huyu kupigwa na kuumizwa vibaya serikali ya kijiji
ilimkimbiza
hospitali Teule ya ifisi na kwamba hali ya afya yake si nzuri hali
iliyopelekea
mke wake aitwaye Kristina Kyando (45) Kuzirai,”alisema
Hata
hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alithibitisha
kutokea
kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi litahakikisha linawatia mbaroni
watu
wote waliohusika na mauaji hayo.
Kumeibuka
kwa vitendo vya madereva pikipiki kujichukulia sheria mkononi ambapo
hivi
karibuni walifunga barabara ya Iwambi Jijini Mbeya kwa kulishinikiza
jeshi la
polisi kuwaachia watuhumiwa wawili ambao walituhumiwa kuiba pikipiki
ili
wawaue.
Mwisho.
Picha na Ezekia Kamanga
kutoka mbeya
|
Hakuna maoni
Chapisha Maoni