Zinazobamba

NAPE ATIMIZA AHADI, HUKO NYAMONGO

1_cba88.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akifafanua jambo wakati wa kikao maalum cha ndani na wakazi wa eneo la Nyamongo, ambapo wananchi wa eneo hilo walikuwa wakieleza kero zao na wamiliki wa mgodi wa North Mara
2_0ca9e.jpg
Ndugu Elizabeth Malembela akielezea jinsi utaratibu ulivyombovu wa kuwahamisha na kuwalipa fidia wakazi wanaoishi kando kando ya mgodi wa North Mara.
3_c97d0.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisikiliza kwa makini malalamiko ya wananchi wa Nyamongo juu ya ukiukwaji wa utaratibu na mikataba baina ya wawekezaji na Wanavijiji.(P.T)
5_72600.jpg
Mkuu wa Wilaya ya Tarime Ndugu John Henjewele akiwaelezea wakazi wa Nyamongo kazi za kikosi kazi (Task force) katika kurahisisha shughuli za kutathimini ardhi na kuchukua malalamiko ya wananchi dhidi ya wawekezaji wa mgodi wa North Mara.
7_56e25.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi  Nape Nnauye akiangalia moja ya eneo linaloaminika kutiririsha maji yenye kemikali kutoka kwenye Mgodi wa North Mara kwenda kwenye mto Mara na kuhatarisha afya za wananchi.
8_1ef56.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiangalia kwa karibu kabisa maji ya kemikali kutoka machimbo ya mgodi wa North Mara kuelekea mtoni.
9_efccb.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisoma jiwe la msingi la ofisi ya Kikundi cha Bodaboda Nyamongo mara baada ya kuzindua ofisi hiyo.
11_38a33.jpg
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime Ndugu Amos Sagara Nyabikwi akihutubia wakazi wa Nyamongo wakati wa mkutano wa hadhara ambao Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye aliwaelezea wananchi wa eneo hilo hatua za awali za kutafuta ufumbuzi wa matatizo yao zilivyoanza.
14_8ec63.jpg
Mkurugenzi wa Kushughulikia Malalamiko dhidi ya Jeshi la Polisi,Magereza,Uhamiaji,Zimamoto na Uokoaji Ndugu Agustine D. Shio akihutubia wananchi wa Nyamongo na kuwaambia amesikia malalamiko yao dhidi ya Jeshi la Polisi na atalifanyia kazi mapema iwezekanavyo na haki zitapatina.
12_24017.jpg
Sehemu ya Wakazi wa Nyamongo wakisikiliza kwa makini hotuba ya Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi nape Nnauye.
13_6b5f4.jpg
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nauye akihutubia wakazi wa Nyamongo wilayani Tarime na kuwaelezea jinsi alivyoanza rasmi kazi ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili wananchi wa Nyamongo

Hakuna maoni