MAMA SALMA KIKWETE KUKUTANA NA JAMII YA WAMASAI JIJINI DAR, LENGO NI KUWAAMBIA UKIMWI UPOOOO
MAMA SALMA KIKWETE ANATARAJIWA KUWA MGENI RASMI KATIKA MKUTANO UTAKAOWAKUTANISHA JAMII YA KIMASAI HAPA NCHINI, MKUTANO UTAKAOFANYIKA MAPEPMA HIYO KESHO PALE MWL. NYERERE CONVETION CENTRE
LENGO KUU LA MKUTANO HUO NI KUWAHUSISHA JAMII YA KIMASAI KATIKA KUZUIA MAAMBUKIZI YA UKIMWI,KUBORESHA AFYA YA UZAZI PAMOJA NA KUIMARISHA NA KUENDELEZA USTAWI WA WASICHANA NA JAMII NZIMA YA WAFUGAJI
TAARIFA ZILIZOZIFIKIA FULLHABARI NI KWAMBA, WARSHA HIYO YA SIKU MOJA INALENGA KUWALETA PAMOJA JAMII YA OLOIBONI NA WASAIDIZI WAKE PAMOJA NA LAIGWENANI AMBAO NI VIONGOZI WA KIMILA WA NGAZI ZA JUU KABISA WA JAMII YA KIMASAI ILI KUPEWA ELIMU YA UKIMWI
AKIZUNGUMZA NA FULLHABARIBLOG, KATIBU MTENDAJI WA TAASISI YA WANAWAKE WAMA BW. DAUDI NASIBU AMESEMA MKUTANO HUO NI MUHIMU SANA KWA MUSTAKABALI WA JAMII YA KIMASAI HIVYO WANATEGEMEA VIONGOZI WA JAMII YA KIMASAI WATAONYESHA USHIRIKIANO
Hakuna maoni
Chapisha Maoni