Afisa upelelezi wa wilaya Mbeya mtatiro
akishukuru wakazi wa mtaa wa iyela kwa ushirikiano utulivu
waliouonyesha wakati wa zoezi la kutafuta vidhibiti.
Kijana
Daniel Kossam (21) anatuhumiwa wa kumuua bosi wake Bi,Pelesi Chaula
(32)ambaye alikuwa akiishinaye nyumba moja huko mtaa wa Ilembo kata ya
Iyela
mkoani mbeya
Daniel
alikuwa akiuza duka la vifaa vya pikipiki la bi, Pelesi lijulikanalo
kwa
jina la 'Twiyanze' lililopo kijiji cha Mbalizi nje kidogo ya jiji la
Mbeya.
Chanzo
cha ugonvi inadaiwa kuwa ni kuchelewa kurudi nyumbani kijana huyo ndipo
Pelesi
alipochukua jukumu la kumuuliza jambo lililozua ugonvi katiyao na
kusababisha
kifo cha bi.Pelesi Chaula.
Kifo
cha marehemu Pelesi kimetokana na kupigwa na kitu chenye ncha kali
mwilini
mwake.
Wakati
mauaji hayo yanafanyika mume wa bi Pelesi Chaula alikuwa safarini
wilayani
Makete mkoani Iringa.
Baada
ya mauaji hayo Kijana Daniel alichukua simu mbili za marehemu na simu
yake
pamoja na fedha kiasi cha 114000/= na kuzitumbukiza chooni kisha
alienda
kwa jirani kuwajulisha kuwa walikuwa wamevamiwa na majambazi na kwamba
wamemuua
bosi wake huyo.
Majirani
walipofika eneo la tukio walishangaa kuona kuwa hakuana sehemu ya nyumba
iliyokuwa
imevunjwa, walipo muuliza Daniel alijibu kuwa alisahau kufunga milango,
baaada
ya majibu hayo waliingiwa na mashaka na kuamua kutoa taarifa polisi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi Mjumbe wa serikali ya mtaa Bi,Neema
Mwasampeta
alisema,' Dan alichelewa kurudi na alifokewa sana,nadhani hicho ndiyo
chanzo cha ugonvi wao'. aliongeza kuwa alimjua kijana huyo kwa muda wa
mwaka
mmoja.
|
No comments
Post a Comment