TATOA WAJIPANGA KUMSHITAKI MAGUFURI, WADAI AMEWASABABISHIA HASARA KUBWA
Pinda amponza Waziri Magufuli

Waziri Mkuu Mizengo Pinda (Kulia) akizungumza jambo wa waziri wa Ujenzi
John Pombe Magufuli.Waziri Mkuu amempongeza Magufuli kwa jitihada zake
za kuondoa kero barabarani
Na Hadija Jumanne.Mwananchi
Kwa ufupi
Chama hicho kimesema hasara hiyo imekuja baada ya
kutoa agizo kwa wamiliki wa magari makubwa ya mizigo kutozwa asilimia
tano kwa kila gari litakalozidisha uzito na kuagiza kurudiwa kwa
utaratibu wa zamani wa msamaha wa asilimia tano ya tozo hiyo.
Pia kimesema Serikali imepoteza zaidi ya Sh30 bilioni kutokana na mgomo wa siku tano.
Chama hicho kimesema hasara hiyo imekuja baada ya
kutoa agizo kwa wamiliki wa magari makubwa ya mizigo kutozwa asilimia
tano kwa kila gari litakalozidisha uzito na kuagiza kurudiwa kwa
utaratibu wa zamani wa msamaha wa asilimia tano ya tozo hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, kwa niaba
ya Chama cha Wamiliki wa Malori nchini, Mkurugenzi wa Kampuni ya
Usafirishaji ya Simba, Azim Dewji , alisema chama chake sasa kinafanya
mahesabu ili kujua hasara ambayo kila kampuni imepata katika kipindi cha
mgomo.
Alisema baada ya hatua hiyo, wamiliki wa malori watachukua hatua za kisheria dhidi ya waziri huyo.
Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Waziri Mkuu,
Mizengo Pinda, kufuta agizo lililotolewa na Dk Magufuli la kuwataka
wamiliki wa magari makubwa ya mizigo kutozwa asilimia tano kwa kila
gari, litakalozidisha uzito.
Dewji alisema sekta ya usafirishaji ni sekta
muhimu katika kukuza uchumi kwa kuwa inaajiri watu zaidi ya milioni moja
sawa na mara nne ya wapigakura wa Waziri Magufuli hivyo, hakupaswa
kutumia ubabe kwenye suala hilo.
Dewji alisema Waziri Magufuli alipaswa kupelekwa
kwenye propaganda za chama kwa sababu ndio sehemu inayomfaa kwa ajili ya
kupiga propaganda na sio kuwa waziri.
No comments
Post a Comment