Zinazobamba

MKURUGENZI WA BENKI AFUNGUKA, ASEMA WATANZANIA WANAOGOPA KUKOPA, ADAI ASILIMIA 80 YA WATANZANIA WOTE HAWATUMII HUDUMA ZA KIBENKI, AWATAKA WAACHE UWOGA

 HAYO YAMESEMWA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA POSTA HAPA NCHINI BW. SABASABA MOSHIRINGI WAKATI AKIWAHUTUMIA WAJASILIAMALI  WALIOHUDHULIA MAFUNZO ELEKEZI KWA WAJASILIAMALI YALIYOFANYIKA MAPEMA HII LEO
MKURUGENZI WA BENKI YA POSTA BW. SABASABA MOSHIRINGI AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WAJASILIAMALI, MASHIRINGI AMEWATAKA WAJASILIAMALI HAO KUACHA UWOGA, KWANI UWOGA UNARUDISHA NYUMA MAENDELEO YAO
AKIZUNGUMZA NA WAJASILIAMALI HAO, MKURUGENZI HUYO AMESEMA HALI ILIVYO SASA HAIRIDHISHI HATA KIDOGO KWANI WATUMIAJI WA HUDUMA ZA KIBENKI BADO IKO CHINI NA KWAMBA ILI KUTATUA HALI YA UMAIKINI INAYOWAKABILI WATANZANIA WALIO WENGI HATUNA BUDI KUKUBALI KUKOPA KWANI HIYO NDIYO NJIA SAHIHI YA KUJIINUA KIUCHUMI

BW. MOSHIRINGI AMEONGEZA KUSEMA KUWA HAKUNA NAMNA YA KUWEZA KUJIONGEZA UCHUMI WETU KAMA HATUKO TAYARI KUKOPA, HATA WENZETU WA NCHI ZILIZOENDELEA WAMEKUWA WAKIKOPA KATIKA KUENDELEZA MIRADI MBALIMBALI YA BIASHARA ZAO

WAJASILIAMALI WAKIFUATILIA KWA KARIBU MAFUNZO ELEKEZI YALIYOTOLEWA KWAO MAPEMA HII LEO JIJINI DARESALAAM

MKURUGENZI MTENDAJI WA BENKI YA POSTA AKIWA SAMBAMBA NA MGENI RASMI KATIKA MAFUNZO HAYO, MH. NAIBU WAZIRI WA VIWANDA PAMOJA NA MWENYEKITI WA BODI WA BENKI HIYO BI. LETICIA RUTASHOBYA

WAJASILIAMALI WAKIBADILISHANA MAWAZO,

No comments