Zinazobamba

MKAPA AWATAKA VIJANA KUJENGA TABIA YA KUSOMA, ASEMA NI NJIA PEKEE YA KUONGEZA MAARIFA,


VIJANA  WAMETAKIWA KUJENGA TABIA YA KUJISOMEA VITABU MBALIMBALI  KAMA VILE VYA HADITHI, VYA KIHISTORIA NA VINGINE VINGI ILI WAWEZE KUWA NA UWEZO WA KUPAMBAMBANUA MAMBO MBALIMBALI YANAYOWAKABILI,

WITO HUO UMETOLEWA NA RAISI MSTAAFU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANI MH. BENJAMINI WILLIAM MKAPA WAKATI AKIZINDUA MRADI WA  KUHAMASISHA VIJANA KUJISOMEA MAPEMA HII LEO JIJINI DARESALAAM,

MKAPA AMESEMA KUWA WATANZANIA KWA UJUMLA WAMEKUWA HAWANA HALI YA KUJISOMEA VITABU MBALIMBALI NA BADALA YAKE SASA VIJANA WETU NAO WAMEJIKITA KATIKA MITANDAO YA KIJAA HUKU WAKIACHA VITABU MUHIMU VYA KUPANUA UWEZO WAO WAKUELEWA MAMBO MBALIMBALI,

"SOMENI VITABU MTAKUWA NA UELEWA MZURI, SOMENI KITABU KAMA CHA AKINA SHABANI ROBERT, NG'UNGI WA THIONG'O NA VINGINE VINGI ILI MUUONGEZE MAARIFA "ALIONGEZA MH. MKAPA

RAIS MSTAAFU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKIWASOMEA MOJA YA KITABU WATOTO WA SHULE YA MSINGI WALIOHUDHULIA KATIKA UZINDUZI WA KAMPENI YA KUWAFANYA WATANZANIA WAWE NA TABIA YA KUJISOMEA,


WAWAKILISHI WA WANAFUNZI WA SHULE MBALIMBALI WAKISIKILIZA KWA MAKINI BABU YAO AMBAYE NI RAISI MSTAAFU WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AKIWASOMEA MOJA YA KITABU VILIVYOLETWA KATIKA UZINDUZI HUO

MKURUGENZI WA MRADI HUO AKIWA PAMOJA NA MSHEREHESHAJI KATIKA SHUGHULI HIYO, WAKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WADAU WALIOHUDHULIA KATIKA HAFLA HIYO ILIYOFANYIKA KATIKA MAKTABA YA TAIFA JIJI DARESALAAM

MKAPA AKIWA NA WADAU MBALIMBALI WALIHUDHULIA HAFLA HIYO     




No comments