Zinazobamba

MAUAJI YA MWINIMSANGA,MKE WA MAREHEMU AMSHUMTU KAMISHINA KOVA KOVA KWA KUUKANA UKWELI



Hivi karibuni kamishina wa polisi kanda maalum ya daresalaam DCP Suleimani Kova aliitisha mkutano na waandhsi wa habari kuzungumzia mauaji ya Kijana Suleimani  Mwinyimsanga aliuawa kinyama usiku wa julai 19 huku muuaji halisi akiwa bado hajatambulika

Akizungumza katika mkutano huo kamishina ametangaza kifo cha Bw. Suleimani lakini akishindwa kuthibishwa kuwa jeshi lake ndilo chanzo kikubwa cha kifo cha mtu huyo ambaye mwili wake umekutwa na majeraha makubwa ya kupigwa sehemu zote za mwili wake wakati ukioshwa kiasi cha kufikia baadhi ya viongo vyake kuvunjwa vunjwa
KAMISHINA WA POLISI KANDA MAALUM YA DARESAALAAM AKIWA KATIKA MOJA YA MIKUTANO YAKE NA WAANDISHI WA HABARI, KOVA AMESEMA HANA HAKIKA KAMA JESHI LAKE LIMESHIRIKI KATIKA MAUAJI YA KIJANA HUYO

Kamishina kova, kwa mujibu wa maelezo ya Mtoto wa marehemu,Jophrey Issa ambaye amekili kuwa  kushuhudia askari wako wakimpiga Bw. Suleimani huku wakimtaka aonyeshe kitu asichokijua, wakati walipompeleka nyumbani kwake kwa niaba ya  kukagua uwepo wa walichotaka kumtuhumu nacho katika mchana huo wa julai 19 iweje leo hii useme wanajeshi wako hawajaweza kuhusika na mauaji ya kijana huyo

 Lingine kamishina wangu wa kanda maalum ambayo ama hakika inashughulika na mambo maalum kama mwenyewe ulivyozoea kusema, baada ya kifo cha Bw. Sulimani pia mmetangaza kupatikana kwa silaha ambayo ilidhaniwa kuwepo nyumbani kwa Bw. Selemani, je silaha hiyo ilipatikana mikoni mwa nani na ni kwanini mlichukua hatua ya kuficha maiti ya Mwinyimsanga kwa muda wa siku tano,mlikuwa mnataka kufanyia kazi gain hasa?

MKE WA MAREHEMU BI HONORATA GIDO AKIWA MWENYE HUZUNI NJE YA OFISI KITUO CHA SHERIA, MAMA HUYO ALIENDA KUOMBA MSAADA WA KISHERIA MAMA HUYO ANADAI MUME WAKE AMEULIWA KINYAMA NA JESHI LA POLISI.
Ama hakika nina maswali mengi sana ambayo kwa sasa najiuliza kuhusu mauaji ya Mtanzania huyu ambaye hata kama ni kweli mualifu lakini haki ya kutoa uhai wake wameipata wapi

Ikumbukwe kuwa kwa sasa familia yake inalia na kusaga meno, mtu wao muhimu ambaye alikuwa anafanya kila liwezekanalo ili watoto wake waweze kwenda shule  tayari ameshaporwa uhai wake, unadhani nini hasa kitatokea katika familia hiii, hili ni swali pia ambalo ninajiuliza

Kamishina wangu wa kanda maalum, sasa nimeshudia leo hii jeshi lako likipelekwa kituo cha haki za binadamu wakishutumu jeshi lako kushiriki katika mauaji ya Bw. Selemani Mwinyimsanga

Kwa uelewa wangu mdogo hatua hiyo ni mwanzo wa kuchafua heshima yako iliyojengeka kwa kipindi cha miaka mingi ya utumishi wako ambao mpaka leo wananchi wa jiji la Daresalaam wamekuwa wakikupigia upatu kuwa unafanya vizuri sana katika suala zima la utendaji kazi,
Katika kupeleka malalamiko hayo ya msingi, Mke wa Marehemu Bi.Honorata Gido amesema wameamua kufikia hatua hiyo baada ya kugundua kuwa jeshi la polisi halina nia njema na familia hiyo, kwani kwanza kabisa walificha maiti ya mume wake kwa kipindi cha siku tano katika hospitari ya mwananyamala, pili wamempiga mume wake kwa kosa ambalo halikuthibishwa mahakamani na tatu kuondoa uhai wa mtu wamekiuka katiba na sheria ya jeshi la polisi wanaloliongoza

TUNAWASILI RASMI KUIONYESHA DUNIA KUWA TUMEONEWAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!,NDIVYO WANAVYOELEKEA KUSEMA NDG. WA MAREHEMU SELEMANI MWINYIMSANGA KUSHOTO AKIWA NA MTOTO ALIYESHUHIDIA BABA YAKE AKIPIGWA NA JESHI LA POLISI WAKIWASILI OFISI ZA KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU MAPEMA HII LEO

Naye kwa upande wake Mlezi ambaye ameteuliwa na familia ya Bw. Selemani Mwinyimsanga kusimamia suala hilo kwa sasa Bw.Joachim Mgembe amebainisha wazi kuwa jeshi la polisi halina sababu ya kukataa kuhusika na mauaji ya kijana wao kwani kila dalili na ushahidi upo wa kuthibitishwa mauaji  hayo yalliyofanywa na polisi

Polisi wapo kwa kulinda wananchi kama inafikia hatua mtu mmoja anachukua sheria mkononi mwake na kuua bila mtuhumiwa kuthibishwa mahakamani hapo kuna tatizo na ndio maana tumekuja kitua cha haki za binadamu kulilia haki ya kijana wetu Bw. Selemani Mwinyimsanga

Kwa upande wake kova amekana kuwa jeshi lake limeshiriki kwa mauaji ya kijana huyo lakini ameunda tume ya kuchunguza mauaji ya kijana huyo na watu waliohusika waweze kuchukuliwa hatua mara moja
“sina hakika kama ni kweli jeshi langu lihusika na mauaji ya Bw. Selemani lakini nanachoweza sema ni kwamba ninaunda tume kuchunguza suala hilo na kama ikigundulika kuwa askari amehusika na mauaji hayo atachukuliwa hatua au kama kuna raia yeyote ambaye amehusika katika mauaji hayo naye atashughulikiw” alisema Kamishina DCP Suleimani Kova


JOACHIM MGEMBE AKIWA NA MKE WA MAREHEMU BI. HONORATA GIDO, WAKIPOZI KWA PICHA BAADA YA KUFIKA KATIKA KITUO HICHO, WANANDUGU HAO WAMEFIKA KATIKA KITUO HICHO ILI KULILIA HAKI ZA NDUGU YAO BW. SELEMANI

HAPA WAKIWA NJE BAADA YA KUTOA MALALAMIKO YAO








.

No comments