JUKWAA LASEMA UCHAGUZI ZIMBABWE ULIKUWA WA HAKI,HAUKUWA WA UKATILI KAMA WA 2008
| KIONGOZI WA MSAFARA WA JUKWAA LA KATIBA TANZANIABI AISHA ABDULA AKIFAFANUA JAMBO MBELE YA WAANDISHI WA HABARI. ASHA AMESEMA UCHAGUZI ULIKUWA HURU NA HAKIIIIIIIIIIII,KUSHOTO KWAKE NI EBRONI MWAKAGENDA AMBAYE NI MJUMBE WA BARAZA HILO. |
JUKWAA la katiba Tanzania limesifu mchakato mzima wa uchaguzi wa nchini zimbabwe ulivyoendeshwa na kusema kuwa mchakato huo ulikuwa wa utulivu mshikamano na amani katika maeneo yote ya nchi hiyo ikilinganishwa na uchaguzi wa mwaka 2008
Akizungumza
na waandihsi wa habari ofisini kwake mwemyekiti wa jukwaa hilo Bw.
Deusi Kibamba amesema katika uchaguzi huo ambao wao walialikwa kama
waangalizi wa nje waliweza kuangalia katika majimbo yote makubwa ya
nchini Zimbabwe na kubaini uwepo wa hali ya utulivu, mshikamano na amani
katika maeneo hayo.
Majimbo ambayo waangalizi wa jukwaa la katiba
walifanikiwa kuhudhulia na kujionea mchakato wa upigaji kula ni pamoja
na majimbo ya Mashonaland (Harare),Matebeleland (Bulawayo) na Manicaland
(Mutare) ambako majimbo yote hayo kumeonekana hali ya amani ikitawala
Katika
hatua nyingine Bw. Kibamba ametaja baadhi ya kasoro ndogondogo ambazo
zimejitokeza katika uchaguzi huo ili Tanzania kama nchi ambayo pia
tutafanya uchaguzi mwaka 2015 tuweze kujifunza kutoka kwao na kuchukua
hatua stahiki kabla hatujafika siku ya uchaguzi
Miongoni
mwa kasoro hizo ni pamoja na kuchapishwa karatasi nyingi za kupigia
kura kuliko idadi kamili ya walioandikishwa kupiga kura,hivyo kuongeza
dhana ya wizi wa kula kwa vyama vya upinzani
No comments
Post a Comment