SEMINA JUU YA MATUMIZI YA MITANDAO KUFANYIKA MORO,JUMLA YA WADAU 150 KUSHIRIKI PALE NASHERA HOTELI
Naibu waziri wa mawasilano sayannsi
na teknolojia MH. JANUARY MAKAMBA
atafungua semina ya uasalama wa matumiz ya komputa na mitandao yake
katika nyanja zote.
Semina hiyo imeandaliwa
na Taasisi ya ISACA Tanzania kwa kushirikiana na NRD EAST AFRICA ,semina hiyo ijulikanayo kama Cyber defense east africa 2013 itawashirikisha watu
zaidi ya 150 itafanyika kwa siku tatu kuanzia
tarehe 28 mpaka 30 mwezi wa nane katika mji wa morogoro.
Akizungumza na blogu hii rais wa ISACAT TANZANIA ndugu
Boniface Francis Kanemba alisema kuwa semina hiyo italenga kwa kina kutoa
mafunzo kwa wataalamu wa TECHNOHAMA haswa wale wanaohusika na uasalam a wa
mitandao hiyo kutoka pande zote mbalimbali za dunia yakiwemo makampuni kutoka nchi za ulaya ,amerika na afrika
kusini.

Kanemba alisema kuwa wataalamu hao wataonyesha kwa vitendo
mambo mbalimbali yanayofanyika wakati wa kufanya wizi wa mitandao na washiriki
wa semina hiyo watashiriki kwa vitendo hivyo ambavyo vimelenga kutoa ufahamu
zaidi juu ya kile kinachotokea kwenye mtandao haswa kwa matumizi mabaya kama
wizi
Vilevile kila mshiriki atajionea kwa macho yake jin si wizi
wa mtandao unavyoandaliwa na kufanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo katika
mabenki,serikali ,makampuni ya simu na mengineyo na hivyo kuongeza ufahamu wa
jinsi ya kudhibiti uhalifu.
“mafunzo haya ni kwa ajili ya wadau mbalimbali kutoka sekta
zote za umma na binafsi pia kutoka nchi zote tano za afrika mashariki yaani
tanzaia,kenya,uganda ,rwanda na burundi ,hii ni kutokana na nchi hizi kuwa na
changamoto sawa la ongezeko la wizi wa mtandao na matumizi mabaya ya mitandao
katika miaka ya hivi karibuni” alisema ndugu Kanemba
Aidha kanemba alisema kuwa tafiti iliyofanywa na kampuni ya
Deloitte mwaka 2012 inaonyesha kuwa mabenki ya biahsra kwenye inchi za afrika
mashariki yanapoteza takribani zaidi ya shilingi bilioni 80 kutokana na wizi wa
mitandao kwa mwaka kiasi ambacho bado kinasadikiwa kuwa kinaweza kuwa zaidi ya
ikizingatia juwa matukio mengi huwa hayaripotiwi hivyo kutokuwa na idadi kamili
ya fedha zote.
.
No comments
Post a Comment