Zinazobamba

AMESCO TRUCK PARTS YASHINDA TUZO YA BEST BRAND AWARDS 2026


Kampuni ya uuzaji na usambazaji wa vifaa (vipuri) vya magari ya AMESCO Truck Parts,imeibuka kidedea kwenye usiku wa tuzo za best brands 2026 kama kampuni bora ya Mwaka ya uuzaji wa vifaa hivyo.

Tuzo hiyo imekabidhiwa kwa kampuni hiyo kwa niaba ya Waziri wa viwanda na baishara,Judith Kapinga na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo,Bw Aristides Mbwasi kwenye hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam Novemba 13,2026 kama sehemu ya kutambua chapa bora sokoni.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi wa kampuni ya Amesco truck Parts,Bw Amiri Mkufya amewashukuru watanzania kwa kuendelea kuwa na imani na kampuni hiyo na kuipigia kura kwa kishindo,jambo lililopelekea kuibuka washindi.

"kwetu sisi hii siyo tuzo tuu ya kusheherekea mafanikio,bali inatufanya kuongeza chachu ya utoaji huduma na bidhaa zenye ubora na kuwa chapa namba moja barani Afrika,ubora wa bidhaa zetu utaendelea kama sehemu muhimu kwenye kampuni yetu"amesema Bw. Mkufya.Tuzo za Best Brand zimeandaliwa na kampuni ya Best Brand Africa inayoongozwa na Zakayo Shushu,zinatambua kampuni zinazofanya vizuri sokoni na kupendwa na watu (people's choice).

No comments