KATAMBI ASAINI KANUNI KUDHIBITI VING’ORA BARABARANI*
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi amesaini Kanuni za Ving'ora, Ishara zinazosikika na Vimulimuli za mwaka 2026 ili kudhibiti matumizi ya sauti katika Vyombo vya Usafiri.
Waziri Katambi amesema hayo leo mkoani Kilimanjaro wakati akizungumza na Uongozi wa Chama cha Mapinduzi(CCM),Mkoani Kilimanjaro ambako amewasili leo kwa ziara ya kikazi.
“Kila mtu amekua na king’ora kwa hiyo imekua familia ya kambare,ukinunua gari yako unaweka king’ora,bodaboda ina king’ora sasa shughuli hazitaenda ikiwa kila sehemu ni ving’ora tu,sasa ving’ora vitatumika kwa utaratibu maalumu unaotambuliwa na sheria”amesema Waziri Katambi.

No comments
Post a Comment