Zinazobamba

TTCL YAONGOZA UTOAJI WA HUDUMA ZA MAWASILIANAO

Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeendelea kuwekeza katika miundombinu ya mawasiliano pamoja na mifumo ya ndani na nje kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa wateja na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma.

Akizungumza kuhusu maboresho hayo, Mbanguka amesema uwekezaji huo umeiwezesha TTCL kuendelea kutoa huduma bora za mawasiliano kwa wananchi, huku ikiimarisha mifumo inayowezesha kuwahudumia wateja kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

"TTCL imekuwa kinara katika utoaji wa huduma bora za mawasiliano. Haya yote yanawezekana kutokana na miundombinu ambayo tumeiboresha zaidi, lakini pia uwekezaji katika mifumo ya ndani na mifumo ya nje ya namna ya kuwahudumia wateja wetu kwa urahisi na unafuu zaidi,” amesema Mbanguka.

Amesema shirika hilo litaendelea kuboresha miundombinu yake ili kuhakikisha huduma za mawasiliano zinawafikia wananchi katika maeneo mbalimbali nchini, sambamba na kuimarisha mifumo ya huduma kwa wateja.

Mbanguka ameongeza kuwa maboresho hayo yataendelea kufanyika kwa kuhakikisha mifumo inayosaidia utoaji wa huduma inawekwa na kukamilishwa kwa wakati, ili TTCL iendelee kutoa huduma bora, za haraka na zenye ufanisi kwa wateja wake.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za TTCL katika kuimarisha huduma za mawasiliano nchini, huku ikilenga kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya wananchi na taasisi katika matumizi ya teknolojia na huduma za kidijitali.

No comments