LP PAD TRADING CO. LIMITED YATANGAZA RASMI UPATIKANAJI WA LP PADS NCHINI TANZANIA, YAMTAMBULISHA QUEEN MASANJA KUWA BALOZI
Kampuni ya LP PAD TRADING CO. LIMITED inayojihusisha na usambazaji na uuzaji wa taulo za kike zenye ubora wa hali ya juu, leo imetangaza rasmi kuanza kwa upatikanaji wa bidhaa zake za LP PADS nchini Tanzania.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Martini Kadinda, amesema kuwa kampuni inalenga kuwatambulisha Watanzania bidhaa za LP PADS, kueleza dhamira yake ya kuchangia afya na usafi wa hedhi kwa wanawake na wasichana, pamoja na kuhakikisha bidhaa bora zinapatikana kwa urahisi katika maeneo mbalimbali nchini.
Pamoja na hilo, leo pia tunamtambulisha mrembo wetu Queen Masanja kama Balozi wetu mpya. Kupitia kazi zake za sanaa, amekuwa akiwashawishi na kuwavutia mabinti wengi. Tunaamini kupitia yeye, bidhaa yetu ya LP PADS itawafikia mabinti hao wengi.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Balozi wa LP PADS, Queen Masanja, amesema kuwa akiwa balozi mpya wa LP PADS atahakikisha anahamasisha afya, usafi na ustawi wa wanawake na wasichana wa Tanzania.
"Nikiwa kama balozi mpya wa LP PADS, ninafuraha kuwa sehemu ya safari hii muhimu ya kuhamasisha afya, usafi na ustawi wa wanawake na wasichana wa Tanzania. LP PADS ni zaidi ya bidhaa, ni mchango katika kuhakikisha kila mwanamke anapata taulo za kike zenye ubora wa hali ya juu kwa bei nafuu na kwa urahisi," amesema Masanja.
Sanjari na uzinduzi huo, LP PAD TRADING CO. LIMITED inatangaza fursa kwa mawakala wa biashara, wasambazaji na wafanyabiashara kutoka mikoa yote ya Tanzania kushirikiana na kampuni hiyo ili kurahisisha upatikanaji wa LP PADS katika kila kona ya nchi.
Kwa upande wake, kampuni pia imejipanga kuchangia ukuaji wa uchumi kwa kuendelea kuunda ajira kwa Watanzania kupitia shughuli zake za usambazaji, masoko na mauzo ya bidhaa zake.
LP PAD TRADING CO. LIMITED inaamini kuwa upatikanaji wa taulo za kike bora ni haki ya msingi kwa kila mwanamke na msichana, na itaendelea kufanya kazi kwa karibu na wadau mbalimbali kuhakikisha lengo hilo linafikiwa.
Kwa maelezo zaidi kuhusu usambazaji, uwakala na ushirikiano wa kibiashara, wadau wanakaribishwa kuwasiliana na LP PAD TRADING CO. LIMITED.
"YOUR DAY OUR COMFORT"

No comments
Post a Comment