Zinazobamba

SHIGONGO AWAKUMBUSHA VIJANA KUWA WAZALENDO.

*Awataka kutumia rasilimali zilizoachwa na waasisi wa Taifa kwa ajili ya maendeleo

Na Mussa Augustine.

Mbunge wa Jimbo la Buchosa Mkoani Mwanza Shigongo Erick amewasihi vijana wa kitanzania kuwa wazalendo pamoja na kutumia rasilimali zilizopo katika kuliletea Taifa  maendeleo.

Shigongo ametoa rai hiyo leo Aprili 10,2026 jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari kando ya halfa ya uzinduzi wa jukwaa la vijana(Vijana Platform)lililoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam kwa lengo la kuwakutanisha vijana ili kupata taarifa mbalimbali zinazowahusu kwa ajili ya kujipatia maendeleo.


"Nimekuja hapa kuzungumza na vijana kuhusu uzalendo wao,umuhimu wa kupenda Taifa lao,kupenda nchi yao,mwaka 1961 tulipopata uhuru wa nchi yetu tulikua na vijana ambao waliamua kuweka hofu na uoga pembeni,wakaacha kumuogopa mzungu wakasimama imara kudai uhuru wa nchi yao."amesema Shigongo 
Nakuongeza kuwa,"Tanzania ni nchi tajiri mno,nimezungumza mara nyingi na nitaendelea kusema kila siku,wazee wetu hawa walijua chini ya ardhi kuna Uranium,almasi,dhahabu,gesi,Tanzanite,kulikua na utajiri mwingi sana chini ya ardhi baada ya kupata uhuru,lakini wakasema hatutautumia utajiri huu sisi watakuja wautumie watoto wetu."
Amesema kwamba kazi iliyopo kwa vijana wa sasa ni kulitoa Taifa hapa lilipo,kutumia rasilimali zilizopo kuzitumia kulipeleka Taifa mbele dhidi ya maadui kuiondoa nchi kwenye umaskini,maladhi,ujinga,ambayo ndio ilikua vita kubwa kwa waasisi wa Taifa.

"Sisi vijana tuliopo hapa leo tunatakiwa kutumia utajiri wetu ambao wazee wetu waliopigania tukaupata kwa ajili ya vizazi vinavyokuja"amesema Shigongo.

No comments