NONDO ASEMA BAJETI YA VIJANA BADO INA VIZUIZI VYA KUWAINUA KIUCHUMI
Na Mussa Augustine.
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdul Nondo, ameibuka na kuikataa bajeti ya Wizara ya Vijana ambayo imepitushwa bungeni.
Nondo akizungumza leo April 22,2026 na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, amesema bajeti hiyo haijakidhi mahitaji ya vijana hususan katika masala ya mikopo katika kundi hilo.
"Hii bajeti ambayo imepitushwa na Bunge haiwasaidii vijana kwani pesa nyingi zimekwenda kwenye posho za vikao pamoja na safari huku mahitaji ya vijani hususan mikopo ikipewa asilimia ndogo," amesema.
Ameongeza kuwa wataendelea kuipinga bajeti hiyo hadi pale itakapofanyiwa marekebisho na zaidi vijana watakapowekewa bajeti kubwa.
Aidha amesema kuwa kuanzishwa kwa benki ya Maendeleo kwa vijana sio suluhisho kiuchumi kwa vijana,bali Serikali inapaswa kuondoa vizuizi ikiwemo suala la TIN number kwa vijana ambao hawajaanizsha bishara,pamoja na kuwepo kwa uratibu mzuri na taarifa sahahihi za uwekezaji.

No comments
Post a Comment