Zinazobamba

Vijana 521 wapata ajira nje ya nchi,45 waenda Ulaya.

Na Mussa Augustine:

Serikali imeendelea kufungua na kuimarisha njia salama za uhamiaji wa nguvu kazi kwa kushirikiana na nchi rafiki pamoja na taasisi za kikanda na kimataifa,ikiwa ni juhudi za kuhakikisha Watanzania wanapata ajira zenye staha, kulindwa haki zao na kushiriki kikamilifu katika uchumi wa dunia.


Akizungumza katika hafla ya kuwaaga vijana 521 waliopata fursa za ajira nje ya nchi, iliyofanyika Machi 27, 2026 jijini Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -Kazi, Ajira na Mahusiano, Mheshimiwa Deus Sangu, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maono ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kukuza ajira kwa vijana.

Amesema Serikali imejipanga kuhakikisha usalama wa Watanzania wanaokwenda kufanya kazi nje ya nchi unalindwa kikamilifu, na kuwahakikishia vijana hao kuwa waende kwa utulivu na kujiamini kwa kuwa Serikali ipo pamoja nao.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Ajira, Bi. Jane Sologo, aliwashukuru mawakala binafsi kwa mchango wao mkubwa katika kuwaunganisha Watanzania na ajira za nje.
Naye Mwenyekiti wa Umoja wa Mawakala Tanzania, Bw. Abdallah Khaled Mohamed, aliipongeza Serikali kwa ushirikiano wake na mawakala hao, akisema hatua hiyo imeongeza ufanisi na uaminifu katika usimamizi wa ajira za nje.

Halikadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya UCDP kutafuta ajira nje ya nchi  Patrick Kawogo amesema kuwa vijana hao wanaweza kuchangia maendeleo kwenye Taifa leo kupitia ajira zao.
"Tunaunganisha vijana na fursa za ajira na mafunzo kazi nje ya nchi kwenye nchi tofauti tofauti,nchi kubwa ambazo tumewaunganisha ni Marekani,Canada na nchi za Skaninavia ambazo ni Ujerumani,Norway,Denimark na Netherland"amesema Patrick

Nakuongeza kwamba "mafunzo ambayo tunawaunganisha vijana kwa mwaka mmoja na kuendelea ni kwenye maeneo ya Kilimo,(Utalii(Tourism hospitality),pamoja na uhandisi(Engineering?),na hii imekua fursa kubwa sana kwa vijana wa Kitanzania kutokana changamoto za uhaba wa ajira Nchini.


No comments