Serikali Kuifanya Tanzania Kitovu cha Biashara - Dkt. Yonazi
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi amesema Serikali imefanya juhudi mbalimbali za Kisera, Sheria na Kimkakati ili kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki na Kati.
Dkt. Yonazi aliyasema hayo katika kikao cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara cha Baraza la Taifa la Biashara TNBC kilichofanyika jijini Dar es salaam.
Alisema Serikali imefanya jitihada za kukuza biashara nchini huku akizitaka sekta binafsi kuendelea kushirikiana na serikali.
“Serikali imefanya juhudi mbalimbali katika uwekezaji nchini ikiwemo mazingira ya ufanyaji wa biashara ya kisera, kisheria na lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara Afrika mashariki na kati.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. Godwill Wanga alisema kikao hicho kimefanyika ili kujadili maendeleo ya biashara nchini.
Alisema kikao hicho kimejadili vivutio ambavyo serikali inaweza kufanya uwekezaji zaidi katika sekta ya afya ili bima ya afya kwa wote itakapoanza iweze kuwa na faida kwa Watanzania.
“Kikao hichi ni muendelezo wa vikao ambavyo tumekuwa tukifanya mara kwa mara katika kujadili maendeleo ya biashara ambapo katika kikao hiki kimejadili kuhusu miundombinu ya mtandao katika katika nchi yetu.
Aliongeza kuwa :”Tumekubaliana kufanya utafiti kuhusu madhara ya vita katika mashariki ya kati katika uchumi wetu.





No comments
Post a Comment