Zinazobamba

SERIKALI YATENGA BILLIONI 13 KUWEZESHA UJENZI WA OFISI ZA TMA

Na Mwandishi wetu

NAIBU Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, David Kihenzile, ametembelea ujenzi wa ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zilizopo Sinza Simu 2000, jijini Dar es Salaam. Ujenzi huu, unaofadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, unalenga kuongeza ufanisi wa utoaji wa taarifa sahihi za hali ya hewa.

Akizungumza katika ziara hiyo,Naibu Waziri wa Uchukuzi,David Kihenzile amesema Serikali ya Awamu ya Sita imetenga takribani shilingi bilioni 13 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi za TMA.

Kihenzile amesema majengo yote mawili, yaliyoanza kujengwa mwaka 2023 na 2025, yanatarajiwa kukamilika kabla ya mwisho wa mwaka huu. Ameeleza kuwa miradi hiyo itaongeza ufanisi katika utoaji wa taarifa za hali ya hewa na kuwawezesha wataalamu kufanya kazi katika mazingira bora na ya kisasa.

Aidha ameipongeza TMA kwa kumchagua mkandarasi wa ndani, Chuo cha DIT (Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam), kutekeleza miradi hiyo akieleza kuwa hatua hiyo inachochea maendeleo ya wataalamu na taasisi za ndani.

Pia, amewahimiza TMA kutoa taarifa kwa wakati ili kuwasaidia wananchi katika shughuli za kila siku zikiwemo usafiri, kilimo na matumizi ya bahari na amewahimiza wananchi kuendelea kuamini na kutumia taarifa rasmi za hali ya hewa kutoka TMA

No comments