DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUPOOZA UMEME-MKATA
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa kupooza umeme uliopo Mkata mkoani Tanga ambao chenye uwezo wa 2X60MVA 132/33kV, pamoja na ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 45 kutoka kituo cha Mkata kwenda kijiji cha Kwamsisi
Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa gharama ya Shilingi Bilioni 44.14 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme na Shilingi Bilioni 5.75 kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusambaza umeme.
Mradi huo ni miongoni mwa miradi ya uimarishaji wa Gridi ya Taifa wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Wilaya za Handeni na Kilindi pamoja na kuimairisha hali ya upatikanaji wa umeme katika Migodi ya Graphite katika Kijiji cha Kwamsisi.




No comments
Post a Comment