Zinazobamba

DIWANI ZUBERI AMEWAOMBA WANANCHI KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA MABUSHA.

*Amshukuru Dkt Samia kwa kuboresha sekta ya Afya.

Na Mwandishi Wetu.Dar es salaam 

Diwani wa Kata ya Kilakala,Manispaa ya Temeke Mh.Erick Magowa Zuberi amewaomba  wananchi wa kata hiyo kuendelea kujitokeza kwa wingi katika zoezi la upimaji wa mabusha linaloendelea katika Zahanati ya Kilakala ili waweze kupata matibabu.

Mh.Zuberi ametoa wito huo Januari 6,2026 wakati akizungumza na Waandishi wa habari nakufafanua kuwa zoezi hilo la upimaji wa mabusha  limeanza januari tangu 5 na litafikia tamati januari 30,mwaka huu.

"Tumepata bahati kwenye Wilaya yetu ya Temeke katika hospitali yetu ya kata ya Kilakala,kuna zoezi la opresheni bure ya mabusha kutoka Wizarani,tumepata huduma hiyo ambayo kuanzia tarehe 5 mpaka tarehe 30 watu wanakua wanajiandikisha,wale wanaofaa kufanyiwa opresheni basi opresheni hizo zitaanza siku ya ijumaa."amesema 

Nakuongeza kuwa "mwitikio ni mzuri tunaendelea kutoa wito watu waendelee kuja kupata huduma hiyo ambayo ni bure,hadi sasa tumepata watu 75 ambao wamekuja kujiandikisha nakupata vipimo,na wapo ambao tayari ni zaidi ya hamsini (50)wamepita kwenye zoezi la kufanyiwa opresheni itakayoanza siku ya ijumaa." 

Aidha Diwani huyo amemshukuru mheshimiwa rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa madai kuwa zile siku mia moja (100)ambazo vipaumbele ambavyo ameviweka tayari vinafanyiwa kazi ikiwemo kwenye huduma ya Afya ambapo aliweka naziri kuwa ndani ya siku mia moja(100)kuna baadhi ya mambo ikiwemo mambo ya bima ya Afya,na mambo ya kuzuia maiti yatafanyiwa kazi haraka iwezekanavyo.

Katika hatua nyingine Diwani Mh.Zuberi amesema kwamba Sekta ya Elimu katani humo inaendelea vizuri ambapo kata hiyo ina shule tatu ambazo ambapo shule mbili ni Msingi na shule moja ni Sekondari,nakwamba uandikishwaji wa watoto kuanza masomo mwaka huu  unaendelea vizuri. 

"Uandikishaji wa watoto wanaoanza darasa la kwanza umeanza tarehe 5,na taratibu zingine zinaendelea,wito wangu kwa wazazi na walezi wawapeleke watoto wanaostahili kwenda kuanza shule,kwahiyo mimi kama diwani wa kata ya Kilakala natoa wito kwa wazazi wote wapeleke watoto wao wasichana na wavulana wapate elimu ya msingi. 

No comments