MKURUGENZI MKUU TAA ATEMBELEA BANDA LA TMA KATIKA MAONESHO YA NANENANE*
Agosti 6, 2025
Mkurugenz Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Abdul Mombokaleo, ametembelea banda la TMA na kupata elimu ya masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za uandaaji wa utabiri wa hali ya hewa, usambazaji wake na elimu kuhusu Chuo cha Taifa cha Hali ya Hewa www.nmtc.ac.tz
TMA imeendelea kupokea wageni na wadau wa hali ya hewa katika banda la maonesho ya kitaifa ya nanenane 2025 yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma na kutoa elimu juu ya huduma zake.
Maonesho haya yamebeba kaulimbiu:
"Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025"
No comments
Post a Comment