Zinazobamba

KIBUDA ACHUKUA FOMU KUGOMBEA UDIWANI KATA YA TANDIKA.


Na Mwandishi Wetu.

Salum Abdallah Tindwa maarufu kama "Kibuda" amechukua fomu ya kugombea nafasi ya udiwani katika kata ya Tandika kupitia chama cha wakulima (AAFP).

Akizungumza mapema leo August 21,2025 mara baada ya kuchukua barua ya udhamini kutoka Ofisi za AAFP kwa ajili ya kwenda kuchukua fomu katika Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Tandika,Kibuda amesema kuwa ameamua kugombea udiwani kata ya Tandika ili kuondoa kero mbalimbali zinazowakabili Wananchi.
Aidha amesema kuwa changamoto kubwa katika kata ya Tandika ni pamoja na kukithiri kwa vitendo vya uhalifu ambavyo uongozi uliokuwepo madarakani umeshindwa kutafuta mwarobaini wa kukomesha vitendo hivyo.
"Nimeona Maendeleo ya Tandika sio  mazuri kwa wagombea waliopita,kwanza ulinzi sio mzuri,watu wana nyanyasika,na wengine kudhalilika kwenye masuala ya mikopo wakati uongozi uliokuwepo ulishindwa kusimamia hili jambo"amesema Kibuda.





No comments