Zinazobamba

KAMATI KUU CCM YAMPITISHA MASABURI KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KIVULE



Na Mwandishi Wetu

CHAMA  Cha Mapinduzi (CCM)kimempitisha mwanachama  wa ambaye pia aliwahi kuwa Naibu instahiki Meya wa  Halmashauri ya Manispaa ya ilala Ojambi Didas Masaburi kuwa  Mgombea ubunge wa Jimbo la Kivule  jijini Dar es Salaam katika Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.

Masaburi ambaye aliongoza katika mchakato wa kura za maoni ndani ya Chama hicho ametangazwa kuwa mgombea ubunge katika Jimbo hilo  baada ya Kamati Kuu ya CCM kukaa kikao chake jijini Dodoma na kuchuja majina ya wagombea ubunge wake ambao watapeperusha bendera katika Uchaguzi huo.

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) CPA Amoss Makalla ametangaza majina ya wagombea ubunge katika majimbo yote ambapo katika  jimbo la Kivule Mgombea ubunge aliyepitishwa na Chama hicho    ni Ojambi Masaburi .

Baada ya kupitishwa kwa jina lake Masaburi atachukua fomu ya kugombea ubunge na kisha kuirejesha katika Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) na hatimae kusubiria kampeni kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi katika Jimbo la Kivule.

Kwa kukumbusha tu Jimbo la Kivule ni Jimbo jipya ambalo limepatikana baada ya Tume Huru ya Uchaguzi kuligawa Jimbo la Ukonga na kupatikana majimbo mawili  ambayo  Ukonga na Kivule na Jimbo hilo la Kivule Mgombea wake ni Masaburi.

No comments