Zinazobamba

BURAH AMEAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO ZA ZINAZOWAKABILI WANANCHI WA KATA YA KIWALANI


Na Mwandishi wetu

Mgombea udiwani wa Kata ya Kiwalani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Iddi Bura, ameahidi kutatua changamoto sugu zinazowakabili wakazi wa kata hiyo, hasa katika miundombinu ya barabara za ndani ya mitaa, huduma za afya, maji na elimu.

Akizungumza leo Agosti 15, 2025 jijini Dar es Salaam, mara baada ya kukabidhiwa barua ya uteuzi na Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Sylvester Yaredi, Bura amesema changamoto ya barabara za mitaani ni kero kubwa kwa wananchi, hasa kipindi cha mvua.

“Serikali imetuletea barabara za lami lakini barabara za ndani ya mitaa bado ni changamoto. Mvua ikinyesha hazipitiki, nitaweka nguvu kubwa kuhakikisha zinatengenezwa ili kurahisisha maisha ya wananchi,” alisema Bura.

Aidha, ameahidi kuweka mkazo kwenye sekta ya afya, elimu na maji, akisisitiza kuwa anayo dhamira ya kweli ya kuwatumikia wananchi kwa bidii na uadilifu ili kuleta maendeleo ya kweli.

“Ninajua changamoto za Kiwalani, na nimejipanga kuzitatua. Naomba wananchi waniamini kama ambavyo Chama changu kilivyoniamini ili kwa pamoja tufanikishe mageuzi ya kweli katika kata yetu,” amesema Burah

No comments