TANZANIA INAFANYA VIZURI KWENYE SEKTA YA FILAMU.:AMIRY
Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania(TAFF) Rajab Amiry ameshiriki Mkutano wa siku tatu nchini Uganda ambao ulikuwa mahususi kujadili kutengeneza Muungano wakua na soko la pamoja la Filamu Afrika Mashariki.
Akizungumza Juni 11,2025 mara baada ya kuwasili kutoka Nchini Uganda,rais huyo wa Shirikisho la Filamu Tanzania amesema kwamba Mkutano huo ulikuwa na malengo ya kutengeneza muungano wa makubaliano ya zaidi ya nchi nane,kutangaza kazi za filamu kupitia mradi wa Steam Afrika.
Aidha amesema kwamba kwenye mkutano huo wamejadili namna gani wanaweza kupata masoko makubwa ya kuuza Filamu,na pia baada ya kujadiliana na kukubaliana kuweka utaratibu mzuri wa kuingia makubaliano(MOU) ambayo yatasaidia filamu za Afrika kua katika sehemu mzuri kimasoko.
" Tunashukuru Serikali ya Uganda ambayo ilikuwa sehemu ya dhamana ya UNESCO kwa ajili ya kufadhili Tanzania kwa kutuamini na kuwepo bodi ya filamu kwa kuwakilisha ,lakini pia wawakilishi kitoka Zanzibar walikuwepo katika mkutano huo"amesema Amiry
Hata hivyo rais wa shirikisho la Filamu Rajab Amiri amesema sambamba na hilo imepelekea kukutana na marais wengine wa shirikisho,hivyo itapelekea kufungua milango mingine katika soko la filamu haswa kwa waigizaji nchini,nakuwahimiza wajiandae kupata matunda mazuri.
"Tulitaka kujua wenzetu wana nini,na wao ili wapate kuungana na kushirikiana kwa pamoja ili kukuza soko la filamu katika soko la kimataifa."amesema Amiry
Nakuongeza kuwa" Tukiwaangalia wenzetu kama Korea,China wamekua kwa kiasi kikubwa katika soko la biashara ya Filamu, kwa sababu waliungana na kushirikiana.
Ametoa rai kwa Tanzania kuendelea kushirikiana wao kwa wao na kujiaminisha kama wanaweza wanakoelekea.
Kwa upande wake Afisa filamu kutoka Bodi ya Filamu Nchini Ally Makata ameongeza kuwa lengo kubwa kama bodi ya filamu ni kuhakikisha wanaleta maendelea katika tasnia ya filamu na Michezo ya kuigiza
"Ikumbukwe kuwa michezo ya kuigiza na filamu imekuwa biashara na ajira kwa watu wengi hivyo ikatufanya ushiriki Mkutano huo ili kuwepo na makubaliano ambayo ni kujenga uwezo,na masoko,
yaliyozungumzwa ni yale ya ( Stream East) itakuwa app yenye lengo la kutengeneza kazi zenye ubora kwa wasanii ilikuweza kupata masoko nje na ndani ya Afrika" amesema Makata
Aidha mkutano huo ulihudhuriwa na nchi zaidi ya nane ambazo ni Tanzani, Uganda, Kenya, Ethiopia, Malawi,Zambia, Rwanda.
No comments
Post a Comment