Zinazobamba

PURA KUUNGA MKONO KWA VITENDO AGENDA YA MATUMIZI YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA.


Na Mussa Augustine.

Mkurugenzi Mkuu wa  Mamlaka ya Mkondo wa Juu wa Petroli(PURA)Mhandisi Charles Sangweni amesema kuwa Mamlaka hiyo inafanya kazi kwa vitendo kuhakikisha haimuangushi Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika agenda ya Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Taarifa hiyo ameitoa leo Julai 9,2025 Jijini Dar es salaam wakati alipotembelea Banda la PURa kwenye maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara  ( Sabasaba) yanayofanyika katika Viwanja Julius Kambarage Nyerere,ambayo yameanza Juni 28,2025 na yanafikia tamati Julai 13 Mwaka huu.


"Tunafahamu kuwa hii agenda ya Matumizi ya Nishati safi ya kupikia  kinara wake ni Mkuu wetu wa nchi  Dkt.Samia Suluhu Hassan,kwahiyo inanipa faraja sisi  watendaji wake tunafanya kazi kwa vitendo na hatumuangushi mheshimiwa Rais" amesema Mhandisi Sangweni 

Nakuongeza kuwa kwamba kazi kubwa ya  PURA ni  kukusanya data kwa ajiri ya kuangalia upatikanaji wa mafuta,ambapo kampeni ya kwanza ilifanyika katika maeneo ya bahari kuu 2018,tulichimba kisima kimoja, na kampeni kubwa ilikuwa katika maeneo ya uchimbaji kati ya wafanyakazi  150 tulikuwa na wafanyakazi 52 kwa mara ya kwanza kutoka ndani ya nchi na wengi walikuwa wamepata uzoefu kutoka nchi mbalimbali na miradi ya  ndani ya nchi.

Aidha amesema kuwa kwa sasa wanakampeni inayoendelea,ambapo watachimba visima vitatu Mkoani Mtwara ,nakwamba shirika la Petroli Nchini (TPDC )limeshiriki kwa 40% huku asilimia  60% zilizobaki zinafanwya na kampuni ya  nje ya nchi"amesema.

Aidha amefafanua kuwa kati ya makampuni kumi ambayo yanapatiwa tenda ya kufanya  kazi kwenye miradi hiyo,PURA itahakikisha zaidi ya kampuni sita zitakuwa za kitanzania ili kuhakikisha watanzania wanafaidika na miradi hiyo. 

Hata hivyo amehitimisha kwa kusema kuwa kumekuwa na  mwamko mkubwa wa wananchi kutembelea katika banda la PURA,na kuuliza mswali ya kisomi zaidi  ambayo maswali hayo yanaonesha wananchi wamekuwa na mwamko mkubwa kuhusiana na sekta ya Mafuta na Gesi.

No comments