Zinazobamba

Latra CCC yawakumbusha Wananchi kutimiza wajibu wao wakati wa kusafiri.

Na Mussa Augustine.

Wananchi wanaosafiri masafa marefu wamekumbushwa kutimiza wajibu wao wa  kuhakikisha wanatafuta taarifa sahihi nakufanya malipo sahihi ya tiketi,pamoja na kuwa na tiketi halali inayosoma majina yao sahihi ili waweze kupata haki zao pindi changamoto inapojitokeza ikiwemo chombo kupata hitilafu wakiwa safarini.

Hayo yamesemwa leo Julai 9,2025 Jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa huduma za usafiri Ardhini( Latra CCC) Daudi Daudi wakati akizungumza kwenye banda la Baraza hilo lililopo kwenye maonyesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayofanyika katika Viwanja vya Julius Kambarage Nyerere.

"Kitu kikubwa ambacho tunakifanya kwenye maonyesho haya ni kutoa Elimu kwa jamii kwasababu tunakutana na watu wengi,pia wanapata fursa ya kutoa maoni yao au changamoto ya mambo yanayoendelea,si kwa Dar es salaam pekee,hata kwa nchi nzima kwasabubu wengine wametoka mikoa mingine."amesema Daudi

Nakuongeza," Katika utoaji wa Elimu tumekua tukiwambia haki zao na wajibu wao kwamba,ni wajibu wao kabla hujasafiri tafuta taarifa sahihi,hakikisha unafanya malipo sahihi ili uweze kupata tiketi ambayo ni halali,inayosomeka majina yako sahihi na pia ionyeshe unatoka wapi na unaenda wapi,ili iwe rahisi kupata haki zako pindi inapotokea changamoto wakati wa kusafiria".
"Daudi amesema kuwa kukosekana kwa taarifa sahihi za abiria kwenye tiketi imekua changamoto kubwa kwasababu endapo tatizo lolote likitokea labda  chombo kimepata hitilafu ikabidi abiria wahamishwe kutoka chombo kimoja kwenda kingine,chombo hicho kitawapokea abiria hao kutokana na zile tiketi, kwasababu lazima wachukue zile tiketi ili baadae waje kumalizana kimahesabu na yule aliyekua anawapa huduma mara ya kwanza. 

"Abiria wengi wamepatwa na changamoto hiyo,mtu anakuambia mimi ofisini waliniambia gari hii inafika labda Kilombero,tumefika Msamvu wanasema ndo mwisho wa safari,sisi kama baraza la ushauri tunapopokea changamoto kama hiyo inatuwia ngumu sana kumsaidia kwasababu ili tumsaidie lazima tuwe na nyaraka za kurejea na waraka wa kusafiria hua ni tiketi,tukikuta tiketi inasema Dar es salaam-Msamvu lakini yeye anenda Kilombero inabidi kutumia busara kumsaidia".amesema Daudi.

Akizungumzia changamoto wanazokumbana nazo abiria wa masafa marefu na wale wanaotumia daladala Mijini Katibu huyo Mtendaji wa Latra CCC amesema kuwa abiria hao wanakunbwa na changamoto mbalimbali ambapo wamekua wakiwasiliana na mamlaka zinazowasimamia watoa huduma hao kuendelea kuwakumbusha kutoa huduma kwa mujibu wa sheria.
"Kuna Changamoto za watu wanaosafiri masafa marefu,kuna changamoto za watu wanaosafiri mijini kwenye daladala, kwahiyo wanaosafiri masafa marefu changamoto zao kubwa ni ile ambapo watu wanapoenda mapumziko katikati ya safari kisheria inatakiwa wapumzike kwa dakika 30 kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali ikiwemo kula Chakula,

lakini wengi wanasema kwamba wanapokua safarini wanapumzika kwa muda mfupi sana, kwahiyo tunaendelea kulichukua hili kama changamoto na tunawasiliana na mamlaka ili waendelee kuwakumbusha watoa huduma waweze kuhakikisha kwamba abiria wanapewa nafasi ya muda mzuri wa kupumzika katikati ya safari kwani pia wanachoka.
Aidha amesema kuwa Changamoto za wasafiri wa mijini kwa daladala,wanakumbwa na changamoto kubwa mbili,ambapo moja ni ile ya kukatisha ruti,kwamba mtu amepanda gari ambayo inaitwa Kariakoo -Gongolamboto lakini ikifika Ukonga abiria wakashuka wengi, akawaona tena abiria wengi wanataka kurudi mjini anageuka,

ambapo mara nyingi hii wanaifanya muda ambao abiria ni wengi,hiyo ni changamoto kubwa  kwani sio kwa daladala za Dar es salaam tu bali kwa Mikoa yote ambayo wamekutana na watu waliofika kwenye baraza hilo kutoa  maoni ambayo wameyachukua watayaweka kwenye ripoti yao. 
Aidha ameongeza kuwa Changamoto nyingine kwenye daladala ni ule muda ambao wasafiri ni wengi,ambapo wanatumia wapiga debe kubadili nauli kihuni,mfano kama ni sehemu ya nauli ya shilingi mia saba(700) wao wanaita kwa elfu moja(1000),

kwasababu abiria tayari wanakua na msongo wanatamani kurejea makwao kuna wanao mudu kulipia lakini wengine wanashindwa kupata usafiri ambao ni haki yao,hivyo Latra CCC linaendelea kuifanyia kazi changamoto hiyo.




No comments