MWAPINGA ATEMA CHECHE,ASEMA CHADEMA WILAYA YA TEMEKE IPO IMARA.
Asisitiza kwamba hakuna mwanachama anaepanga kukihama chama hicho.
Na Mwandishi Wetu.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Wilaya ya Temeke,kimesema kipo salama hakina mgogoro wa aina yoyote huku kikisisitiza kwamba kitaendelea kuunga mkono agenda ya bila mabadiliko hakuna uchaguzi (NO REFORMS NO ELECTION).
Akizungumza mapema leo Mei 13,2025 na waandishi habari jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Temeke, Benitho Mwapinga ,amewatoa hofu wapenzi na wanachama wa chama hicho kuwa chama hicho kinaendelea vizuri nakwamba hakuna mgogoro wowote wa wanachama kukihama chama hicho.
"Nitumie fursa hii kuwatoa hofu wanachama wote,na pia uongozi wote wa CHADEMA Mkoa upo hapa,hauna tofauti,tunaendelea kujenga chama chetu,hatuna mpango wa kuhamia chama kingine amesema Mwapinga.
Aidha amesisitiza kuwa chama hicho Wilaya ya Temeke kinaungana na maazimio ya Mkutano Mkuu wa CHADEMA kuhusu agenda inayoendelea ya bila mabadiliko hakuna uchaguzi "No Reforms No election"kwakuwa agenda hiyo ni ya kurudisha imani ya uchaguzi.
Amesema Chama hicho kilipitia katika kipindi kigumu cha uchaguzi kwenye uchaguzi wa mwaka 2019,2020,pamoja na 2024 ikiwemo kuenguliwa kwa wagombea wake kwa sababu zisizo za msingi.
Akizungumzia kuhusu wagombea wanaotangaza kuhama chama katika maeneo mbalimbali,Mwenyekiti huyo amesema watu hao hawakuwa wanachama wa chama hicho bali ni matapeli wa kisiasa.
Amesema kuhusu uongozi wa chama hicho ngazi ya Wilaya hadi Mkoa kinapewa ushirikiano na uongozi wa juu wa Taifa wa Chadema hivyo upo imara katika mapambano ya kisiasa.
No comments
Post a Comment