Zinazobamba

MAADHIMISHO MIAKA 30 YA VETA KUFANYIKA DAR MACHI 18 HADI 21.


 Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda,akizungumza na Waandishi wa habari

Na Mwandishi Wetu.

Maadhimisho ya miaka 50 ya Mfumo wa Kitaifa wa Serikali ya Taasisi ya Kusimamia Ufundi Stadi pamoja na miaka 30 ya Mamlaka ya elimu na mafunzo ufundi stadi (VETA) yanatarajia kufanyika Machi 18 hadi 21 mwaka huu katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere Jijini Dar es salaam.

Katika maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa.

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es salaam mapema leo Februari 5,2025 na Waziri wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia  Profesa Adolf  Mkenda wakati akizugumza na waandishi wa habari.

Amesema  maadhimisho hayo yamekuja baada ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan,kutaka kukamilisha vyuo vya veta kila mkoa.

“Kwa sasa tupo katika hatua ya mwisho ya kukamilisha chuo Songwe huku vyuo 64 vikiendelea na ujenzi wake lengo ni kuhakikisha kila kijana wa Kitanzania anapata elimu ya ufundi stadi”amesema

Aidha amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazofanywa na wanafunzi wao ikiwemo kupaka rangi majengo ya shule na kuonyesha bunifu zao mbalimbali zinazofanywa .

Waziri huyo amesema katika maadhimisho hayo kutakuwa na shughuli mbalimbali  kuelekea Kilele cha maazimisho hayo ambazo ni pamoja na kutoa huduma kwa jamii zinazoendana na shughuli za ufundi na ufundi stadi.

Profese Mkenda amesema shughuli nyingine ni pamoja na kupaka rangi katika majengo ya umma kama vile hospital na zahanati na kukarabati majengo ya shule.

Pia amesema katika  maadhimisho hayo kutaendeshwa maonesho ya ubunifu na teknolojia  pamoja na  maonesho ya ujuzi pamoja na kutoa vyeti vya heshima Kwa watu mbalimbali kutokana na mchango wao katika shughuli za maendeleo na mafunzo na ufundi stadi.

Hakuna maoni