WAMACHINGA WAPO TAYARI KUFANYA BIASHARA KWA SAA 24 : NAMOTO
Namoto Yusuph Namoto
Na Mussa Augustine
Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam Namoto Yusuph Namoto amesema kwamba Wamachinga wapo tayari kufanya biashara kwa saa 24 kuanzia februari 22,2025 kama ilivyopangwa na Serikali.
Namoto amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kariakoo Jijini Dar es salaam,nakubainisha kuwa wameanza kujiandaa muda mrefu ikiwemo kuimarisha ulinzi katika maeneo mbalimbali ya Kariakoo.
"Mpango huu wa kufanya biashara kwa saa 24 tumeanza kujiandaa muda mrefu,sisi tumeingia mkataba na kampunli ya ulinzi ya Mikumi Security Guard,sasa tuna askari wapatao sabini ambao wanalinda meza za bidhaa za Wamachinga lakini pia kuongeza usalama katika soko letu la Kariakoo,hivyo tumewa link na askari Polisi wa kituo cha Polisi cha Msimbazi "amesema Namoto
Nakuongeza kuwa,"wamekua wakikamata wahalifu,wezi waliokua wanavunja magodauni,stoo za watu lakini pia uchafuzi wa Mazingira kulikua na watu wanajisaidia haja ndogo kwenye mitaro,kulikua na mama lishe ambao wakimaliza shughuli zao walikua,
wanamwaga mabaki ya chakula kwenye mitaro nakuchangia kuziba kwa mitaro,na wale wauza machungwa na madafu walikua wanamwaga uchafu popote nyakati za usiku,kwahiyo tangu tumeweka hii kampuni ya ulinzi ya Mikumi imesaidia sana kulinda usalama katika maeneo hayo.
Amesema kuwa mpango wa Biashara kwa masaa 24 una manufaa makubwa kwa Wamachinga kutokana na kuwepo kwa changamoto ya upatikanaji wa maeneo ya kufanyia Biashara katika jiji la Dar es salaam,hali hiyo itasaidia wale ambao hawana maeneo ya biashara kuweza kufanya biashara zao nyakati za usiku.
"Mpango huu utapunguza biashara holela kwasababu mtu atajua saizi sina nafasi ya kufanya biashara mchana lakini kuanzia saa 12 jioni yule aliyeanza tangu asubuhi amechoka anarudi nyumbani na kundi lingine linaingia,
lakini pia imeongeza wigo wa biashara kwa wenzetu mama lishe na baba lishe na makundi mengine kama vile wauza chips,soda,maji pamoja na maafisa usafirishaji ikiwemo bodaboda na bajiji.
Aidha ameendelea kusema kuwa mpango huo umetoa fursa kwa wamiliki wa nyumba zinazozunguka eneo la kariakoo kutokana nakwamba baadhi ya Wafanyabishara watakodi maeneo ya stoo kwa ajili ya kuhifadhi bidhaa zitakazo uzwa ndani na nje ya Dar es salaam
"Mpango huu pia unagunguza gharama za uendeshaji wa biashara,mfano mtu anaekuja kutoka Mkoani anaweza kuingia hapa saa mbili au saa tatu usiku akafanya manunuzi,akafanya booking SGR na asubuhi akaweza kuondoka, nakupunguza gharama mbalimbali ikiwemo za hotelini ,hivyo naomba mpango huu uratibiwe vizuri una manufaa makubwa" amesisitiza Namoto
"Mpango huu unaenda sambamba na sisi Wamachinga kuanza kufanya usajiri,kuhakiki kanzi data yetu,kuhakiki wale tulio nao na kuanza kufanya mazungumzo na mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) waanze kutupa Elimu na kututengenezea mifumo ambayo mwisho wa safari na sisi tutaanza kulipa kodi kuichangia serikali.
Aidha amesema kuwa oparesheni hiyo inaenda kwapamoja kwa kushirikiana na Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kushughulikia maegesho holela ambayo yanafanya njia za mitaa ya Kariakoo zisipitike kwa urahisi,pamoja na mamlaka ya Maji safi na Maji taka Dar es salaa( DAWASA) kuhakisha inasimamia chemba zinazotoa maji taka kwanye eneo hilo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni