NLD YATOA MSIMAMO WAKE KUELEKEA UCHAGUZI MKUU
Chama Cha National League for Democracy (NLD) kimesisitiza kwamba kitashiriki uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu 2025.
Kauli hiyo imetolewa leo februari 23,2025 na katibu mkuu wa chama hicho Doyo Hassan Doyo wakati akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kamati kuu ya chama hicho uliyofanyika Buguruni, Ilala jijini Dar es salaam.
Aidha Doyo amesema kuwa kufuatia tamko la Mwenyekiti Taifa wa Chadema Tundu Lissu alilolitoa hivi karibuni kua "No reforms, no election" NLD haijaunga mkono msimamo huo, nabadala yake kitawaeleza wananchi sera zake ili waweze kukipa lidhaa ya kushika nafasi mbalimbali za uongozi.
"Vyama vya siasa vipo 19, ikiwemo chetu cha NLD,sisi hatuendi msituni wala hatususii uchaguzi,bali tunaenda kuwaeleza wananchi sera zetu ili watupe lidhaa ya kuwaongoza"amesema Doyo
Akizungumzia kuhusu kujiunga kwa vyama vya upinzani kukabiliana na CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao, Doyo amesema kwamba chama cha NLD ni mhanga wa Muungano wa UKAWA mwaka 2015.
Doyo amesema mwaka 2015,chama cha NLD,CUF,CHADEMA na NCCR-Mageuzi viliungana kuing'oa CCM madarakani lakini NLD ilidhurumiwa kwa kuwaondoa wagombea wake wa nafasi mbalimbali za uchaguzi.
"Hizi kelele zinazopigwa kuhusu kushirikiana ni unafiki,chama kinachokuja kutuambia NLD tujiunge kuiondoa CCM ,chama hicho tunakiona ni adui yetu namba moja kwani hatujanufaika na Muungano wa kisiasa"
Nakuongeza kuwa ,"ili Muungano uwe mzuri lazima sheria ya mgawanyo wa haki kwa vyama vya siasa vilivyoungana baada ya uchaguzi uzingatiwe na uwekwe wazi ili kila chama kinufaike".
Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Mfaume Khamis Hassan wakati akifungua mkutano wa kamati kuu ya chama hicho,ameiomba Serikali inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan kuwapatia ajira ya kudumu walimu wanaojitolea.
Hassan amesema kwamba walimu hao wanafanya kazi kubwa hivyo ni vywema Serikali iwangalie kwa jicho la kipekee iwapatie ajira za kudumu.
Pia mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kuwaasa Watanzania kuendelea kudumisha amani ya nchi,nakuachana na vyama vya siasa ambavyo vimekua vikichochea uvunjifu wa amani Nchini.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo wa NLD amempongeza Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuteuliwa kuwa Mgombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,huku akimtakia kila la kheri katika safari yake hiyo.
Hakuna maoni
Chapisha Maoni