MBUNGE NDAISABA ATEMBELEA MGODI WA BULYANHULU KAHAMA
Na ERNEST RUHUGU*
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Ngara.
Kahama,Shinyanga.
Mbunge wa Jimbo la Ngara *MH.NDAISABA GEORGE RUHORO* ambae ni Mjumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ameshiriki ziara ya kikazi ya kamati ya Nishati na Madini iliyotembelea mgodi wa uchimbaji wa madini ya dhahabu wa BULYANHULU uliopo Kahama mkoani Shinyanga.
Katika zara hiyo *MH RUHORO* amejifunza na kushuhudia uwekezaji mkubwa katika sekta ya madini unaofanywa na *Dr. SAMIA SULUHU HASSAN* Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye mgodi huo kupitia kampuni ya Serikali ya *TWIGA MINERAL COOPERATION* na BARRICK ambapo mgodi huo unaingizia Taifa Matrioni ya fedha kupitia tozo, ada, mgao wa faida n.k zinazolipwa Serikalini.
Ushiriki wa Mbunge Ruhoro umefanyika katika wakati mwafaka ambapo kampuni ya *TEMBO NICKEL* ya uchimbaji wa madini ya Nickel yenye muundo unao fanana na muundo wa mgodi wa BULYANHULU unatarajia kuanza. Kama mwakilishi wa wananchi mafunzo aliyoyapata *MH *RUHORO** yataleta tija katika kutengeneza mazingira wezeshi ya kuwasaidia Tembo Nickel kuharakisha ukamilishaji wa maandalizi na hatimaye kuanza kuchimba madini ya Nickel kwa haraka zaidi.
Akiwa huko *MH.RUHORO* amejifunza uwekezaji wa mgodi wa BULYANHULU kwa wananchi kwenye sekta za afya, elimu maarifa na ujuzi, maji, miradi ya kukuza uchumi na kuondoa umasikini kwa wananchi wanaozunguka mgodi wa BULYANHULU mambo ambayo atayasimamia vizuri kwa upande wa TEMBO NICKEL. Hapa wananchi ni kuhakikisha RUHORO wanampatia mi 5 tena ili hizi neema zisipotee.
Kwa mambo makubwa aliyoyaona Mbunge wetu makini, anawashuhudia wananchi wa Ngara na Watanzania wanaosoma taarifa hii kuwa Tanzania imebahatika kupata Rais *DR. SAMIA SULUHU HASSAN* mpenda maendeleo mwenye uchungu na watu wake na anawaomba kumpatia zawadi ya kura nyingi katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka huu 2025.
MBUNGE NDAISABA ATEMBELEA MGODI WA BULYANHULU KAHAMA
Reviewed by mashala
on
16:18:00
Rating: 5

Hakuna maoni
Chapisha Maoni