Zinazobamba

Mbeto asema Pemba si mateka wa upinzani

Na Mwandishi  Maalum, Pemba 

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimevunja mwiko wa kisiasa kudhani  Pemba ni mateka wa upinzani na kwamba wanaweza kufanya watakavyo kwa kuendesha siasa  za kufikirika.

Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Idara ya Itikadi,  Uenezi na Mafunzo ,Khamis  Mbeto  Khamis, ameeleza hayo kufuatia wanachama zaidi  ya 2500 kukihama ACT  Wazalendo na kujiunga CCM .

Mbeto alisema  tokea mwaka 1995,  upinzani  umekuwa ukiifanya  Pemba ni kichaka cha kufanya  siasa za  uongo , kupotosha dunia na kukigeuza kisiwa hicho, shamba la mapato binafsi ya wanasiasa wao  wanaotajirisha.

Alisema kwa muda mrefu Pemba imetumika  kubadili maisha binafsi  ya wanasiasa  wa upinzani wanaochaguliwa   Udiwani , Ubunge na Uwakilishi huku  wawakilishi  hao wakishindwa kutatua  changamoto  za wananchi.

"CCM  kimevunja mwiko wa kuifanya   Pemba mateka wa upinzani . Kuna baadhi ya  wanasiasa walidhani wangeifanya Pemba  watakavyo. Wamewatumia   sana wananchi ili kufikia matlaba yao .Zama hiyo sasa imepita "Alisema Mbeto 

Aidha  aliongeza kusema kuwa  utendaji  wa Serikali  ya awamu ya Nane Zanzibar  chini ya Rais  Dk  Hussein Ali Mwinyi,  imewafumbua macho wananchi wa Unguja na Pemba  sasa wanafurahia mwamko wa maendeleo . 

"Zama ya siasa za kuwagawa wananchi kwa Upemba na Uunguja  imepitwa na wakati. Wazanzibari wanajitambua  ni wamoja na hawatogawanyika au kudanganyika"  Alisema Mbeto 

Pia Katibu huyo Mwenezi , alisema mabadiliko ya miaka minne ya maendekeo toka Rais  Dk Mwinyi awe madarakani ,uongozi wake umeleta mabadiliko makubwa  ya maendeleo yanayoonekana unguja na pemba. 

"Miaka mitano ijayo Rais Dk  Mwinyi  ataifanya za Zanzibar kuwa nchi inayotamaniwa  na kila binadamu kuishi. Maendeleo yake  yataishangaza dunia na kuwa kimbilio la kila mtu aidha kutamani kuishi , kuwekeza miradi  au kutalii" Alisisitiza Mbeto

Hakuna maoni