Mbeto:Upinzani umewakatisha tamaa watanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kushamiri kwa mivutano ,ombwe la uongozi na demokrasia ndani ya vyama vya upinzani huku viongozi wake wakigombana ni ushahidi upinzani hauwezi kuminiwa na watanzania
Pia CCM kimewataka wananchi kuvikwepa vyama hivyo kwakuwa haviko kwa ajili ya hatma ya kujali Amani , Utulivu na Umoja wa Kitaifa .
Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, Idara ya itikadi, Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis , akiwa Bandarini Kisiwani Unguja ,akielekea katika Mkutano Mkuu wa CCM Jijini Dodoma.
Mbeto alisema kujitokeza kwa mitafaruku ya mara kwa mara ya uongozi ,viongozi kuvuana nguo hadharani ni dalili ya kutoaminika kwao mbele ya wananchi.
Alisema viongozi wa upinzani hawafanyi siasa kwa ajili ya kutumikia wananchi ,kutoheshimu matakwa ya katiba zao , bali wapo kwa ajili ya kupigania vyeo na maslahi binafsi .
Alieleza, kuna tofauti kubwa ya kisiasa na kiuongozi kati ya CCM na upinzani, viongozi wa CCM wanajenga heshima ya taasisi yenye kuaminika , inayohimiza umoja na maendeleo, upinzani una kazi ya kubeza kila hatua za kimaendeleo .
"Kugombana kwao na kuadhiriana , huku wakitukanana na kunga'ng'ania madaraka ni wazi upinzani hauna misingi imara ,nidhamu ya vyama vyao ni butu na kutofuata maadili "Alisema Mbeto .
Aidha alisema ni makosa yatakayojutiwa na baadhi ya watu wanaovishabikia vyama hivyo bila kutojua malengo , sera na madhumuni ya kuundwa kwa vyama hivyo .
'Wananchi wasidhani shabaha, sera na malengo ya upinzani yanafanana na CCM. Hamuwezi mkawa na malengo maalum ya kujenga Umoja, Amani na kutumikia wananchi , mkaanza kuvutana wenyewe kwa wenyewe " Alionya Mbeto
Alidai kuna viongozi wa upinzani wameonyesha dalili za udikteta huku baadhi yao wakiwa hawana hekima ,busara na maarifa ya kuogoza hivyo hawafai kuchaguliwa na kuaminiwa.
"CCM kitaendelea kushinda chaguzi zote kwakuwa hakujatokea upinzani unaoaminiwa na wananchiHamuwezi kuwaachia shamba wanyama wahabaribifu mkadhani mtavuna mavuno yenye tija na faida " Alisema Mbeto
Hakuna maoni
Chapisha Maoni