Zinazobamba

*DKT KAZUNGU ATETA NA BALOZI WA TANZANIA ABU DHABI*

 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Dkt Khatibu Kazungu akisalimiana na Balozi wa Tanzania Falme za kiarabu UAE Luteni Jenerali mstaafu Yacoub Hassan Mohamed slipom tem wa kwenye Ubalozi huo mjini Abu Dhabi

📌 *Anadi miradi ya nishati  kuvutia wawekezaji kutoka Abu Dhabi*

📌 *Ashiriki hafla ya ufunguzi wa Wiki ya uendelezaji Nishati Abu Dhabi na utoaji tuzo za umahiri*

📌 *Balozi wa Tanzania Abu Dhabi awataka watanzania kuchangamkia fursa za ajira*

Abu Dhabi, UAE

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia umeme na nishati jadidifu Dkt  Khatibu Kazungu  amekutana na kufanya mazungumzo na  Balozi wa Tanzania Abu Dhabi Mhe. Luteni Jenerali Mstaafu Yacoub Hassan Mohamed alipokwenda kwenye ofisi  za ubalozi huo kumtembelea.

Dkt Kazungu aliambatana na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki Mkutano wa Baraza la 15 la Wakala wa Kimataifa wa Nishati Jadidifu IRENA mjini Abu Dhabi anbapo alimweleza Balozi Yacoub umuhimu wa Tanzania kupata fedha za kutosha kutoka kwa wawekezaji ili iweze kutekeleza miradi ya nishati jadidifu anbayo ni rafiki kwa mazingira na kuepuka athari za mabadiliko ya Tabianchi.

‘’ Tunaishukuru sana Serikali ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi nzuri inayofanya kutoa kipaumbele kwenye utekelezaji wa miradi na sisi kama Wizara ya Nishati tunaahidi kutekeleza kwa vitendo." Alisema Dkt KazunguAwali akizungumza kwenye kikao hicho Balozi wa Tanzania, Abu dhabi Luteni Jenerali Mstaafu Yacoub Hassan Mohamed alisema, Watanzania  wanapaswa kuchangamkia fursa za ajira zilizopo mjini Abu Dhabi kama ilivyo kwa nchi nyingine kama India, Kenya na Uganda ili kuinua uchumi wa nchi na kukuza kipato kwa wananchi wake

Aliipongeza Wizara ya Nishati kupitia TANESCO kwa kazi nzuri inayofanya ya kuhakikisha umeme unakuwepo wa kutosha na wa uhakika hususani kwenye mradi wa treni ya mwendo kasi ambayo umekuwa na tija kwa wananchi na Serikali kwa ujumlaBalozi wa Tanzania  Jenerali mstaafu Yacoub Hassan Hassan Mohamed akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania unaoshiriki mkutano wa baraza la 15 la IRENA Abu Dhabi

"Nitoe rai kwa Watanzania kuwa mabalozi wazuri wa mradi huu wa treni ya SGR pamoja na wataalamu wa TRC na TANESCO kuhakikisha wanafanya kazi kwa pamoja kuhakikisha hakuna hitilafu yoyote na watanzania wafurahie matunda ya mradi huo kutoka kwenye Serikali yao.

Katika hatua nyingine Dkt. Kazungu alishiriki hafla ya ufunguzi wa  wiki ya uendelezaji nishati ikiwa ni mwendelezo wa fursa zilizopo kwenye Baraza Kuu la 15 la IRENA ili kutoa fursa za kubadilishana uzoefu na wawekezaji kwenye maonesho 


hayo.

Hafla hiyo iliambatana na  utoaji wa tuzo za Rais wa umoja wa falme za kiarabu UAE zijulikanazo kama  Zayed Sustainability Prize, kutambua mchango wa makundi mbalimbali yanayoleta mabadiliko chanya kwenye sekta ya nishati ambapo mtanzania kutoka taasisi ya Open Map Development  ameshinda kwenye kipengele cha mabadiliko ya tabianchi.

Mwakilishi wa taasisi ya Open Map Development kutoka Tanzania akipokea Tuzo ya kipengle cha mabadiliko ya tabianchi kutoka kwa taasisi ya Zayed Sustainability  ya mfalme wa UAE

Hakuna maoni