Zinazobamba

PAMBANO LA KNOCKOUT YA MAMA KUFANYIKA DESEMA 26,2024 JIJINI DA ES SALAAM.



Na Mussa Augustine 


Kampuni ya Mafia Boxing imeandaa pambanao la Knockout ya Mama litakalofanyika Desemba 26,2024  katika ukumbi wa Superdome uliyopo Masaki Jijini Dar es salaam.

Pambano hilo litawakutanisha bondia 13 wa Kimataifa kutoka nchi mbalimbali ikiwemo Africa KusiGhana na Malawi ikiwa lengo ni kutoa burudani kwa mashabiki na wapenzi wa mchezo wa masumbwi.

Taarifa hiyo imetolewa Desemba 18,2024 Jijini Dar es salaam Msemaji wa pambano hilo Jimmy Mafufu wakati akizungumza na Waandishi wa habari nakubainisha kwamba maandilizi ya pambano hilo yamekamilika ,nakwamba litatanguliwa na pambano la ufunguzi litakalofanyika Desemba 20,2024 katika ukumbi uliyopo Magomeni usalama ambapo ndipo zilipo Ofisi za Kampuni ya Mafia Boxing.

Aidha Mafufu amesema kwamba mikanda mitano inatarajiwa kugombaniwa siku ya Desemba 26,2024 ikiwemo mkanda wa WBC Africa  ambao tangu Tanzania ipate uhuru mwaka 1961 haujagombaniwa hapa Nchini Tanzania.

"Pambano hili ni maelekezo ya Serikali,kwani Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ameamua kuwekeza kukuza mchezo huu kama anavyofanya kwenye michezo mingine,hivyo tunafuraha kubwa mchezo wa masumbwi umerudi kwenye hadhi yake" amesema Mafufu.

Nakuongeza kuwa "Mchezo huo utakua na mvuto wa aina yake,unakutanisha mabondia wenye uwezo mkubwa ulingoni akiwemo bondia Mchanja na Ibra,hivyo mashabiki na wapenzi wa mchezo wa masumbwi wajitokeze kwa wingi kuweza kushuhudia mapambano hayo ambayo yote yatapigwa kwa wakati mmoja".

Aidha amesema kwamba kingilio katika pambano hilo VVIP shilingi  laki moja( 100,000/=) VIP shilingi elfu hamsini(50,000/=) na Kawaida shilingi elfu ishirini(20,000/) huku meza ya watu kumi ikiwa ni shilingi milioni moja na laki tano( 1,500,000/=).
Kwa upande wao baadhi ya wasanii wa kike wa Bongo Movie akiwemo Chuchu Hans amesema kuwa pambano hilo linaleta burudani kwa Watanzania huku akimpongeza Rais Dr.Samia kwa jitihada za kuwekeza kwenye mchezo huo.

Kauli hiyo imeungwa mkono na waigizaji Wema Sepetu pamoja Shamsa Ford ambapo wamesema kwa nyakati tofauti  kuwa Mchezo wa masumbwi umesaidia kuleta ajira,kwani wanawake na wanaume wenye vipaji vya kupigana wamekua wakijitokeza kwa wingi hali ambayo inawasaidia kujikwamua kiuchumi kupitia mchezo huo.

Kampuni ya Mafia Boxing ni Kampuni ambayo imekua ikishirikiana na Serikali kupitia kampeni yake "Knockout ya Mama" ikiwa lengo ni kuinua mchezo wa masumbwi kama ilivyo kwenye mchezo wa mpira wa miguu kupitia kampeni yake ya "Goli la mama".







Hakuna maoni