Zinazobamba

MTINIKA AMEZIKA TAASISI ZINAZOHUDUMIA WATU ZAIDI YA 100 KUTEKELEZA MAAGIZO YA WAZIRI MKUU MAJALIWA.

Na Mussa Augustine.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa ametoa maagizo ifikapo Desemba 31,2024 ,taasisi zote za Serikali na binafsi ambazo zinahudumia watu zaidi ya miamoja(100)kuacha kutumia nishati chafu ya kupikia nabadala yake zitumie nishati safi na salama.

Hayo yamesemwa Desemba 22,2024 Jijini Dar es salaam na Mstahiki Meya wa Manispaaa ya Temeke Mohamed Mtinika kwenye kilele cha wiki ya Nishati safi na salama iliyoandaliwa na Shirika la Madini la Taifa( STAMICO)katika viwanja vya Mwembe yanga nakuzibainisha taasisi hizo kuwa ni pamoja na Shule,Jeshi la Magereza,Vyuo na Hospitali.

Bw.Mtinika ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw.Albert Chalamila amesema kuwa kwa sasa viongozi kuanzaia ngazi za Mitaa hadi Mkoa wanapaswa kutekeleza maagizo hayo ya Serikali ili kuhakikisha Mazingira yanatunzwa.

"Viongozi wenzangu naomba tutekeleze maagizo haya yaliyotolewa  na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa,Ofisi ya Mkuu wa Mkoa itaanza ukaguzi wa utekelezaji wa agizo hili" hivyo wakuu wa Taasisi hizo hakikisheni mnatakeleza maagizo haya baada ya Desemba  31 mwaka huu".amesisitiza Bw.Mtinika.

Amesema kuwa kwa sasa Dunia inasumbuliwa na hali ya mabadiliko ya tabianchi hivyo zinahitajika jitihada za makusudi kutunza Mazingira na kuachana na ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa  badala yake kutumia nishati safi na salama ikiwemo gesi ya kupikia pamoja na mkaa wa Briquettes ambao unazalishwa na STAMICO kutokana na makaa ya mawe,na hauna madhara yoyote.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO DKt Venance Mwasse amesema kuwa uzalishaji wa mkaa huo utokanao na Makaa ya mawe ni utekelezaji wa agenda ya Kitaifa inayotaka kufikia mwaka 2034 zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi na salama ya kupikia.

Aidha amesema kwamba STAMICO itaendelea kushirikiana kwa ukaribu na wadau wengine ili kuhakikisha matumizi ya nishati safi na salama yanawafikia wananchi wote hapa Nchini na kuunga mkono jitihada za Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kutaka wananchi watumie nishati safi na salama ili kuepuka madhara ya kiafya pamoja na Mazingira.
Awali Bi.Janeth Masaburi ambaye ni mbunge wa viti maalumu ameiomba Serikali kuiongezea STAMICO mitambo ya uchakataji wa mkaa wa Briquettes ili kuweza kuzalisha mkaa mwingi utakaowafikia wananchi wengi.

Hata hivyo amewaomba wananchi kutumia mkaa huo ili kuweza kuondokana na tabia ya kukata miti hivyo kwa ajili ya kuni na mkaa hali ambayo inasababisha uharibifu wa Mazingira pamoja ukame.

"Kizazi hiki kinakata miti hovyo kwa tamaa za fedha,hali ambayo itasababisha  kizazi kijacho kipate madhara makubwa ya kimazingira,naomba wananchi mtumie nishati safi na salama ikiwemo  mkaa wa Briquettes ambao unazalishwa na STAMICO kwani ni rafiki wa Mazingira na hauna madhara ya kiafya" amesem

Hakuna maoni