Zinazobamba

TRA NA ZBS KUSHIRIKIANA UKUSANYAJI WA KODI ZA FORODHA ZANZIBAR.

Na Mussa Augustine.

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Nchini(TRA) Yusufu Mwenda amese itma kuwa usalama wa mizigo inayopitia Zanzibar sasa utaimarika kutokana na TRA kuingia makubaliano ya ushirikiano na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS)ikiwa ni  kurahisisha shughuli za biashara.

Kamishna Mwenda amesema hayo  leo Novemba 5,2024 jijini Dar es Salaam wakati wa kusaini makubaliano hayo na Shirika la Viwango Zanzibar (ZBS) kurahisisha shughuli za biashara zinazotumia  forodha Zanzibar.
Aidha amebainisha kuwa  TRA ina jukumu la kikatiba la kusimamia kodi za forodha katika Jamhuri ya Muungano Tanzania hivyo watashirikiana na ZBS  kubadilishana taarifa mbalimbali kwa kutumia mifumo kabla ya kuruhusu mizigo itoke kwenye bandari za Zanzibar.

Ameendelea kufafanua kuwa  kabla ya kuingia makubaliano hayo mizigo ilikuwa inachukua muda mrefu ambapo kwa sasa muda utapungua na kuondoa vikwazo na urasimu uliokuwepo awali ambao ulikua unasababisha kuchelewesha mizigo kutoka bandarini.

Hata hivyo Kamishna Mkuu huyo wa TRA amesisitiza kuwa mwelekeo wao ni kuwa na makubaliano na taasisi kaguzi zipatazo 13 ili kurahisisha utoaji wa mizigo Zanzibar pamoja  na shughuli za biashara.

"Kupitia makubaliano haya itasaidia Wananchi kutumia bidhaa salama ambazo hazina madhara kwa afya zao, lakini pia TRA itanufaika na ukusanyaji wa Mapato kwa ajili ya kuleta Maendeleo kwa Taifa"amesema Kamishna Mwenda.
Kwa upande wake  Mkurugenzi wa ZBS, Yusuph Majid Nassoro, amesisitiza kuwa hawataruhusu bidhaa yoyote kuingia visiwani humo kama mtu hana namba ya mlipakodi (TIN Number) ili waweze kutambulika na kulipa kodi za Serikali

"Hatuwezi kuruhusu mfanyabiashara yeyote kuingiza bidhaa zake bila Tin number(namba ya mlipakodi),tunataka kila mfanyabiashara alipe kodi stahiki ya serikali" amesema Nassoro

Hakuna maoni